Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo aliyasema hayo katika ukosoaji mkubwa wa sera za rais huyo wa zamani licha ya hatua za mkuu wa Pompeo rais Donald Trump kuamua kuviondoa vikosi vya jeshi la Marekani kutoka Syria.
"Tunahitaji kutambua ukweli huu kwasababu iwapo hatutafanya hivyo, tutafanya makosa ya uchaguzi kwa hivi sasa na hapo baadaye Na uchaguzi wetu , kile tutakachokichagua leo kina athari kwa mataifa na kwa mamilioni ya watu , kwa usalama wetu, kwa ufanisi wa uchumi wetu, kwa uhuru wetu , na ule wa watoto wetu." Alisema Pompeo
Katika hotuba ambayo aliitoa katika chuo kikuu cha Marekani mjini Cairo, Pompeo alijitenga na utamaduni wa kidiplomasia wa Marekani wa kuepuka kutangaza hadharani mizozo wa ndani nchini Marekani kwa kumshambulia Obama katika mahali ambapo mtangulizi huyo wa rais Trum alitoa hotuba ya kihistoria yenye lengo la kuimarisha mahusiano na ulimwengu wa Kiislamu.
Pompeo ameiwasilisha Marekani kuwa ni nguvu ya kufanya mazuri katika mashariki ya kati, na kudokeza kwamba Obama aliiona Marekani kama " nguvu inayoitaabisha mashariki ya kati".
Baadhi ya maafisa wa zamani wa Marekani na wachambuzi wamemshutumu mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani kwa kusoma vibaya historia na kujificha katika mapenzi ya binafsi ya Trump kupunguza jukumu lake katika eneo hilo.
Chanzo:Dw
0 comments:
Post a Comment