Monday, 28 January 2019

RAIS MAGUFULI AMTEUA HAKIMU KESI YA MBOWE, MATIKO KUWA JAJI

...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo jana kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwatangaza baadhi ya majaji wengine wa mahakama ya Rufani na mahakama kuu.

Miongoni mwa Majaji walioteuliwa ni Jaji Wilbard Mashauri ambaye ni Hakimu katika kesi inayowakabili viongozi 6 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia anasimamia kesi inamkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Jamal Malinzi.

Katika kesi ya inayomkabili Freeman Mbowe na Esther Matiko, akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi hao wawili kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.

Kesi nyingine ambayo inasimamiwa na Wilbard Mashauri ambaye kwa sasa ni Jaji, ni kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Godfrey Gugai ambaye anatuhumiwa kwa kutakatisha pesa pamoja na kumiliki mali ambazo haziendani na na kipato chake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

TANGAZO LA TOUR MBUGA YA SAADAN

FUNGUA PAZIA

NDOA ZA UTOTONI

Narudi nyumbani

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger