Thursday 31 January 2019

TUNDU LISSU AMJIBU NDUGAI " BUNGE HALIJAWAHI KUNILIPA HATA SENTI MOJA'

...
Tundu Lissu amesema Bunge la Tanzania halijawahi kutoa hata senti moja kugharamia matibabu yake.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 31, 2019 saa chache tangu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8 milioni zikiwa stahiki zake na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu kwake.

Lissu amekiri kulipwa Sh43 milioni zilizotolewa na wabunge wenzake kama mchango wao na kwamba kiasi kingine alicholipwa kinachofanya jumla ya fedha hizo kufikia Sh250 ni mishahara na stahiki zake, lakini siyo gharama za matibabu.

Ametoa sababu tatu ambazo Spika Ndugai alizitoa Aprili mwaka jana, kwamba Bunge haliwezi kulipia gharama za matibabu yake.

Lissu amezitaja sababu hizo kuwa hawajapata barua ya kibali ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili; hawajapata barua ya kibali cha Katibu Mkuu Wizara ya Afya; na tatu hawajapata barua ya kibali cha Rais (John) Magufuli kuidhinisha malipo hayo.

“Sasa anaposema wamenilipa pesa hizo anapaswa kuulizwa, je, ni lini walipata barua hizo tatu za vibali?” amehoji Lissu na kuongeza:

“Ukweli pekee uliopo ni kwamba Bunge halijawahi kunilipa hata senti moja ya gharama za matibabu yangu. Hata senti moja!”

Na Kalunde Jamal, Mwananchi 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger