Tuesday 29 January 2019

WALIMU WASIMAMISHWA KAZI KWA KUOA WANAFUNZI WAO,WENGINE KUFELISHA MITIHANI

...

Peti Siyame, Mpanda 

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, limewasimamisha kazi walimu wanne shule za msingi, kwa tuhuma za kuoa wanafunzi wao na kuwapatia ujauzito kupisha uchunguzi wa tuhuma zao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo , Raphael Kalinga alisema kuwa walimu hao wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zao.

Pia, baadhi yao uhamisho wao wa kwenda kufundisha katika vituo vingine vya kazi umesitishwa, wakihofiwa kuendelea na ‘ukware’ wao huko. Majina ya walimu hao tunayo.

Kalinga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Machimboni, alibainisha hayo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo kilichoketi jana.

Aidha baraza hilo la madiwani, limewashusha vyeo walimu wakuu wa shule za msingi kumi na kumvua madaraka Ofisa Elimu wa Halmshauri ya Nsimbo (Shule za Msingi), Marcus Nazi baada ya Halmashauri hiyo kuwa na matokeo mabaya ya mitihani ya taifa ya kumaliza elimu ya msingi kwa miaka miwili mfululizo.

“Wakati Nazi alipokuwa Ofisa ELimu Ufundi, Michael Nzyungu alikuwa Ofisa Elimu (Msingi) lakini kwa kipindi chake chote halmashauri haikuwahi kuwa na matokeo mabaya katika Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi .... Tulikuwa nafasi ya pili au ya tatu lakini baada ya kushika nafasi hii tumekuwa na matokeo mabaya sana ... nafasi hii imemshinda, hataendelea tena na kazi hiyo “ alibainisha.

Via Habarileo
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger