Thursday 31 January 2019

KESI YA MBOWE NA MATIKO YAPANGIWA HAKIMU MPYA

...

Kesi inayowakabili baadhi ya viongozi wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa Chadema, imeendelea leo ambapo imepangiwa Hakimu mpya anayejulikana kwa jina la Kelvin Mhina.

Hatua hiyo ya kesi hiyo Na.112/2018 kupangiwa Hakimu mpya imekuja baada ya aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam, Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais Januari 28,2019.

Wakati akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi wawili wa CHADEMA, M/Kiti , Mbowe na Mbunge Esther Matiko kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.

Katika kesi hii ya viongozi wa CHADEMA, Hakimu mpya Kelvin Mhina, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, 2019 itakapotajwa tena baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kutoa taarifa kwamba kesi hiyo ilienda kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa mahakama ya rufaa.

Ameeleza kwamba upande wa mashtaka ulikata rufaa kupinga dhamana hivyo kesi hiyo itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019.

Hata hivyo, Mbowe na Matiko bado wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana.

Chanzo - EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger