Monday 28 January 2019

CHADEMA WATAKA ASKOFU KAKOBE APUUZWE

...
Baada ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship nchini Tanzania, Zachary Kakobe, kuwataka viongozi wa CHADEMA waliotoa maneno machafu kwa viongozi wa dini kutubu haraka iwezekanavyo, baadhi ya viongozi wamemjibu kwamba anapaswa kupuuzwa, yeye ndiye atakayetumbukia kwenye shimo.

Wakati wa Ibada ya jana siku ya Jumapili, Askofu Kakobe alisema kwamba kuna baadhi ya viongozi wa siasa wa CHADEMA tena walioko katika baraza kuu waliwatukana viongozi wa dini kupitia mitandao ya kijamii, hivyo wasipotubu chama chao kitatumbukia kwenye shimo refu.

Kupitia baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii ya viongozi hao akiwepo Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amendika kwamba, "Kama kweli Kakobe ameongea maneno haya , anapasawa kupuuzwa, yeye ndiye ametumbukia kwenye shimo, aliwahi kusema umeme hautawaka pale Serikali ilipopitisha nguzo za umeme nje ya kanisa lake, huyu, aliwahi kusema Mrema atakuwa Rais Huyu, can we trust him anymore,"?.

Ameongeza kwamba, "CHADEMA hatuombi kupendelewa na kiongozi yeyote wa dini, sisi tunataka, utu, demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru wa Mawazo, uhuru wa vyombo vya habari, tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya. Kiongozi yeyote wa Dini asiyetaka haya, amepungukiwa na utukufu wa Mungu".
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini nae amedai kuwa Waziri Hamisi Kigwangalla ndiye anayepaswa kumuomba msamaha Askofu huyo na kwamba yeye ndiye aliyewahi kumtukana.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kwamba, "ni sawa kuheshimu watumishi wa Mungu. Ni baraka zaidi watumishi wa Mungu kumheshimu Mungu kwa dhati, kwa maneno, matendo, tabia na misimamo yao juu ya haki/matendo mema. Utumishi haupimwi kwa idadi ya waumini wala nguo za kitumishi. Ndio maana imeandikwa tutuwajua kwa matendo yenu".
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger