Friday, 11 January 2019

MAHAKAMA YAWAFUTIA KESI KITILYA NA WENZAKE..WARUDISHWA MAHABUHUSU TENA BAADA YA KUACHIWA

...

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya, maofisa wawili wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri lao.

Uamuzi huo umetolewa leo Januari 11, ambapo washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha, na kwamba wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kabla ya kukamatwa tena, Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidiana na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa.

"Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole. Baada ya maelezo hayo,

Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo, hata hivyo walikamatwa mara tu baada ya kuachiwa na kupelekwa tena mahabusu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger