Friday, 11 January 2019

CRISTIANO RONALDO KUCHUNGUZWA TUHUMA ZA UBAKAJI POLISI YATOA WARANTI

...
Polisi mjini Las Vegas wametoa waranti ya kuchunguzwa kwa chembe chembe za vinasaba au DNA ya Cristiano Ronaldo kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubakaji dhidi ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno anayechezea klabu ya Juventus.

Wakili, Peter S. Christiansen, ameiambia BBC Michezo kuwa ombi hilo ''ni la kawaida''.

Jarida la Wall Street limeripoti kuwa waranti hiyo imewasilishwa hivi karibuni katika mfumo wa mahakama ya Italia.


Ronaldo amekanusha kwamba alimshambulia mwanadada Kathryn Mayorga katika mgahawa mmoja mjini Las Vegas hotel mwaka 2009.

''Bwana Ronaldo amekua akishikilia usemi kuwa yale yaliyotokea Las Vegas mwaka 2009 ni mambo ya watu wawili waliyokubaliana, kwa hiyo bila shaka chembe chembe za DNA zitapatikana, kwa hiyo sioni haja ya polisi kutoa ombi hilo kama sehemu ya uchunguzi wao,"ilisema taarifa ya Christiansen.

Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani ambalo lilikuwa la kwanza kuangazia taarifa hiyo mwezi Oktoba, lilisema kuwa Bi Mayorga aliandikisha ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya kufanyika kwa tukio linalodaiwa.

Der Spiegel lilisema kuwa mwaka 2010, Mayogra aliafikiana na Ronaldo kutatua suala hilo nje ya mahakama ambapo alilipwa dola 375,000 ilisizungumza hadharani madai hayo.

Chanzo:Bbc
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger