Maandamano hayo ni changamoto kubwa kwa Rais Omar Al-Bashir jenerali wa zamani wa jeshi ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi 1989 na tangu wakati huo anashinda uchaguzi ambao wapinzani wake wanasema sio wa haki na wala huru
Vikosi vya usalama nchini Sudan vilifyatua gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji katika mji wa Omdurman huko Sudan siku ya Alhamis.
Shahidi mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters katika wiki kadhaa za karibuni za maandamano yanayoipinga serikali yaliyochochewa na malalamiko ya kiuchumi na kisiasa.
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilivishutumu vikosi vya usalama katika mji kwa kusababisha majeraha kwa waandamanaji walioko ndani ya hospitali baada ya maandamano ya Jumatano ambapo watu watatu waliuwawa. Baadhi ya watu waliojeruhiwa katika maandamano hayo walipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Vifo vya Jumatano vimejumuisha idadi ya takribani watu 22 waliouwawa huko Sudan tangu maandamano yalipoanza Disemba 19 mwaka jana wakiwemo wafanyakazi wawili wa usalama kwa mujibu wa idadi iliyotolewa na maafisa.
Mamia ya watu pia wamejeruhiwa na mamia wengine wamekamatwa.Siku ya Alhamis huko Omdurman waandamanaji walizuia mtaa wa 40 kwenye mji huo kabla ya vikosi vya polisi kuwashambulia kwa gesi ya kutoa machozi na kulazimisha wengi kutawanyika kuelekea upande wa pili wa barabara. Hakukuwa na ripoti za haraka kuhusiana na vifo vyovyote vilivyotokea hapo.
Chanzo:Voa
0 comments:
Post a Comment