Tuesday, 22 January 2019

RAIS MAGUFULI AMTAKA BITEKO ASIANGALIE SURA YA MTU.. " UTAZIKWA PEKE YAKO"

...

RAIS John Magufuli amemtaka Waziri wa Madini, Dotto Boteko atekeleze majukumu yake bila kujali sura ya mtu kwa kuwa kaburini atakwenda peke yake.

Amesema, hasiti kumfukuza Waziri wa Madini hata kama ameiongoza Wizara hiyo kwa wiki moja.

Amewataka viongozi wa Wizara hiyo wachukue hatua, wawahamishe wataalamu wizarani na atashangaa kama hilo halitafanyika.

Ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa mashaurino wa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuufunga kesho.

Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Madini Dotto Biteko awe mkali, na kwamba, aliyepita, Angellah Kairuki hakuwa mkali ndiyo maana kampeleka akapumzike Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kairuki ni Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Rais Magufuli amemuagiza Waziri Biteko, Naibu wake, Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Amos Msanjila hiyo ndani ya mwezi mmoja wawe wameweka kamera kwenye ukuta wa Mirerani na wasipofanya hivyo wajiandae kuondoka.

Via Habarileo
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger