Mshindi wa gari la tatu kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa, George Isaya mkazi wa Arusha, akifurahi baada ya kukabidhiwa gari lake. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, Meneja Masoko na Biashara wa TBL Edith Bebwa (kulia) na Afisa Mawasiliano wa TBL Amanda Walter.
Meneja ukuzaji Masoko wa TBL na ABInBev Afrika Mashariki Edith Bebwa (katikati) akimkabidhi ufunguo wa gari mkazi wa Arusha, George Issaya mshindi wa gari la promosheni iliyomalizika ya TBL Kumenoga Tukutane Baa.
**
Mkazi wa Arusha, George Isaya (29) ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID, katika droo ya promosheni ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’leo amekabidhiwa gari katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, alisema gari hilo ndio la mwisho katika promosheni hii iliyodumu kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo pia imewezesha wateja wengine Julitha Kilawe wa Dar es Salaam na Frank Nathan wa Iringa kujishindia magari.
“Kwa niaba ya kampuni ya TBL, nawapongeza wateja wetu wote ambao wameshiriki katika promosheni hii na wale ambao wamefanikiwa kujishindia zawadi kubwa za magari na zawadi nyinginezo ambazo zilikuwa zinatolewa kupitia kununua bia za chapa za bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.”
Akiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa gari lake, George Isaya alisema siku zote tangu apigiwe simu na kupewa habari za kushinda gari alikuwa haamini kama kama ni za kweli, leo baada ya kukabidhiwa gari lake ndio ameamini.
“Ninayo furaha kubwa kuona ndoto yangu ya muda mrefu ya kumiliki gari imetimia kupitia kunywa bia aina ya Kilimanjaro, gari hili litanisaidia kunirahisishia usafiri katika kutekeleza majukumu yangu mbalimbali, nashukuru kampuni ya TBL kwa kubuni promosheni zenye kuleta manufaa kwa wateja wake” alisema George Isaya.
Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, aliwashukuru wateja wote wa TBL kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.
0 comments:
Post a Comment