Thursday, 24 January 2019

ALIYEKATWA MIGUU BAADA YA KUFANYIA TOHARA NA NGARIBA APATA MATUMAINI

...

Matumaini mapya ya mtoto Chistopher Masaka (11) ambaye alikatwa miguu yote mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufanyiwa tohara mwaka 2017 yameanza kurejea.

Christopher, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Mtitaa, alikatwa miguu yote kutokana na ushauri wa madaktari wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Akizungumzia mkasa huo baba mzazi wa mtoto huyo, Elias Masaka wa Kijiji cha Mtitaa, Bahi alisema Christopher alizaliwa akiwa mzima kabisa.

Mara baada ya kutahiriwa na ngariba, kijana huyo alianza kuugua miguu akisema alikuwa akihisi kama kuwa vitu vilivyokuwa vikitembelea kwenye nyayo zake.

Baba huyo alisema kadri muda ulivyosonga, tatizo hilo liliendelea na kufikia hatua ya kuanza kutoa majimaji.

Alisema hata aliporejeshwa kutoka jandoni haikuwezekana tena kupelekwa shule kwani wakati huo alikuwa hawezi kutembea umbali mrefu.

Mzazi huyo alisema hakuwahi kukutana na tatizo kama hilo katika ukoo wao wala katika kijiji chao lakini akasema wanajiuliza ni kwa nini chanzo cha tatizo hilo kianzie wakati wa tohara.

Na Habel Chidawali, Mwananchi
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger