Sunday 21 July 2019

MWANAFUNZI ALIYEFARIKI AKIOGELEA MTO KIDALU SHINYANGA AZIKWA...IMAMU AONYA WANAOFUKUA MAKABURI

...

Imamu wa Msikiti wa Aqswa Mabambasi Ngokolo Manispaa ya Shinyanga,Sheikh Hassan Sultan Hassan akizungumza wakati wa mazishi ya mwanafunzi Mustapha Ibrahim wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bugoyi A.


Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mwili wa Mwanafunzi Mustapha Ibrahim (13) wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bugoyi A mjini Shinyanga aliyefariki dunia wakati akiogelea na watoto wenzake katika mto Kidalu Mjini Shinyanga umezikwa.

Mazishi ya mwanafunzi huyo mkazi wa mtaa wa Mabambasi Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Jumapili Julai 21,2019 kwenye makaburi ya Mbuyuni yaliyopo katika kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wwa mtaa wa Mabambasi,David Nkulila ambaye ni diwani wa kata ya Ndembezi,mtoto huyo alifariki dunia baada ya kuzama katika mto Kidalu unaopita mjini Shinyanga akiwa na watoto wenzake.

"Mtoto aliaga walitoka nyumbani kwenda kuswali lakini akiwa na wenzake wakashawishiana kwenda kuogelea mtoni. Natoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuwa kuwa karibu na watoto kuwa walinzi kwa watoto",alieleza Nkulila.

Akizungumza wakati wa mazishi hayo,Imamu wa Msikiti wa Aqswa Mabambasi Ngokolo manispaa ya Shinyanga,Sheikh Hassan Sultan Hassan ameonya tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ushirikina kwenye makaburi.

"Tumeishi katika hali ya kuzikana pande zote mbili Wakristo na Waislamu bila kuwa na athari zozote katika makaburi,lakini sasa kimejitokeza kitu ambacho hakipendezi katika maadili ya kiutu na kidini kwa ujumla....

"Kumetokea wimbi la watu kuanza kufukua makaburi.Tabia hii kibinadamu,kiutu haipendezi,huu ni ushirikina uliobobea,haupendezi na wala haufai.Makaburi yanapaswa kuheshimiwa....

Kuna kaburi ambalo hivi karibuni tulimzika kijana wetu alikuwa mwalimu wa watoto wa Kiislamu anaitwa Hussein Yusuph,nililetewa taarifa kuwa kaburi lilifukuliwa karibu nusu nzima ya kaburi,waliofuatilia pale hawakuzama zaidi kuhakikisha kama kilichukuliwa kiungo au nguo,hii ni ishara mbaya,inaashiria jambo siyo zuri",alieleza Sheikh Hassan.

Alitoa onyo kwa watu wenye tabia hizo waache tabia za kufukua makaburi na kubainisha kuwa mtu yeyote anayefanya vitendo hivyo hatavumiliwa.

"Tunatoa tahadhari na onyo vile vile kwamba mchezo huu uishie hapo,usijirudie tena,sisi sote tuwe walinzi wa amani kuanzia huko nje hadi maeneo ya makaburini,makaburi ni makazi kama makazi mengine ya wanadamu walio hai",aliongeza Sheikh Hassan.

Mtu yeyote atakayemuona mtu anaenda makaburini akimtilia mashaka au wasiwasi amfuatilie ili ajue anachokifanya hapo makaburini,kama ni mhusika basi atamjua labda anaenda kulifanyia usafi ama kufanya maombi atajua na kama ni njia zingine za kishirikina basi atoe taarifa kwa vyombo husika ikiwemo vyombo vya serikali",aliongeza Sheikh Hassan.
Mazishi ya mwili wa mwanafunzi Mustapha Ibrahim wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bugoyi A mjini Shinyanga aliyefariki dunia wakati akiogelea na watoto wenzake katika mto Kidalu Mjini Shinyanga ukizikwa leo katika makaburi ya Mbuyuni yaliyopo Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mazishi yakiendelea.
Imamu wa Msikiti wa Aqswa Mabambasi Ngokolo Manispaa ya Shinyanga,Sheikh Hassan Sultan Hassan akizungumza wakati wa mazishi ya mwanafunzi Mustapha Ibrahim wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bugoyi A.
Imamu wa Msikiti wa Aqswa Mabambasi Ngokolo Manispaa ya Shinyanga,Sheikh Hassan Sultan Hassan akizungumza wakati wa mazishi ya mwanafunzi Mustapha Ibrahim wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bugoyi A
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger