Sunday 28 July 2019

MBUNGE MCHUMI ASEMA MAMILIONI YA FEDHA YAMETUMIKA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA MAFINGA MJINI

...
 Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi akiongea kwenye mkutano wa jimbo akiwaeleza wapiga kura wake kwa namna gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM kama alivyoahidi wakati wa kumba kura kwa wananchi waliompa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Daudi Yassini akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Mufindi wakati wa upokea taarifa ya utelezaji ya  Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya mufindi wakiwa makini kumsikiliza  Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi wakati alipokuwa akiwasilisha mambo aliyoyafanya katika jimbo hilo kwa miaka mitatu aliyopo madarakani

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi wa jimbo la mafinga mjini wamenufaika na matunda ya miaka mitatu madarakani ya mbunge Cosato Chumi kwa ktekeleza ahadi zake kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015 kwa ujenzi wa Kituo cha afya cha Ihongole, ujenzi wa Madarasa, mabweni na maabara katika shule za Sekondari za Changarawe, Ihongole na JJ Mungai,kushughulikia swala la maji na kufikisha umeme katika Vijiji vyote kumi na moja. 

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo hilo Chumi alisema kuwa miradi ya Maendeleo katika Jimbo hilo ni pamoja na ujenzi wa jengo la kisasa la Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambalo liko katika hatua za mwisho, ujenzi wa matanki ya maji katika Vijiji vya Maduma,  Bumilayinga, Kinyanambo na Changarawe ambako ujenzi wa tanki la ujazo wa lita milioni moja unaendelea.

“Bado kuna changamoto katika baadhi ya maeneo lakini yapo mengi yaliyofanyika ambayo ni wajibu wetu kuyasema tena wazi wazi na kuwaelewesha wananchi kwa kuwa yanaonekana kwa macho na kuwaambia kuwa changamoto zitatuliwa kulingana na muda wake hawezi kutatua changamoto zote kwa pamoja” alisema Chumi


Chumi alisema kuwa alipokuwa anaingia madarakani Mafinga hatukuwa na gari la uhakika la kubebea wagonjwa lakini kwa kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake amefanikisha upatikanaji wa magari matatu ya kubebea wagonjwa (ambulance), vitanda na ultrasounds machine ambayo inasaidia katika kuchunguza magonjwa ya kina mama Wajawazito


“wajibu wa kila mwanachama wa CCM kueleza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa wananchi wote  mwananchi wa jimbo la mafinga atambue kazi kubwa inayofanywa jimboni hapo au kwenye majimbo mengine” alisema Chumi

Aidha Chumi alisema kuwa kuna watu ambao kazi yao ni kubeza na kuwapotosha wananchi kazi zinazofanywa na serikali ya CCM,Sasa waelezeni wananchi kuwa ili kuongeza mapato ambayo yatatusaidia kujenga barabara zetu, umeme kufika kila Kitongoji ndio maana Rais Magufuli akaamua kununua ndege ili watalii wengi watembelee mbuga zetu na sisi tupate fedha

“kukaa kimya na kutoeleza na kutafsri faida kubwa ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya tano,nawaambia ndugu zangu kazi kubwa inafanyika lakini bila sisi wana-CCM kueleza umma wa watanzania, basi ni Sawa na bule au kutupa jiwe gizani bila kujua litamkuta nani” alisema Chumi

Chumi amesema kuwa wapo wanaobeza kwa kuwaambia wananchi kuwa miradi ya ujenzi wa Reli na ununuzi wa ndege  haina tija wakati miradi hiyo  inaenda kuchochea ukuaji wa biashara na sekta binafsi kwa ujumla.

“Anakuja mtu anakuambia Wewe treni ya umeme utapanda lini, na Wewe mwana CCM unakaa kimya, hiyo sio Sawa, mueleze wazi wazi kuwa ili tupate fedha, tunajenga reli ya kisasa ambayo itatumika kusafirisha mizigo kwenda nchi za jirani ambazo hazina Bandari, na sisi tutapata fedha ambazo zitagharamia elimu ya watoto wetu, tutajenga barabara za lami, Tutafikisha umeme kila kona ya Mafinga na nchi yote, tutapata maji ya uhakika” alisema


Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daudi Yasini alimpongeza mbunge huyo kwa kazi aliyoifanya ambayo inaonekana tofauti na kuwa na mbunge wa maneno maneno bila kazi kuonekana.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger