Sunday, 28 July 2019

MWENYEKITI WA UVCCM AWAONYA WANAOIKWAMISHA CCM

...

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, Kheri James amewaonya watu watakaothibitika kwa maneno au matendo katika kutikisa mshikamano wa Chama cha Mapinduzi kwamba watawachukulia hatua.

Kheri James ametoa kauli hiyo jana  wakati wa Uzinduzi wa Kagera ya Kijani uliofanyika katika uwanja wa Hamgembe uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Kheri alisema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao katika kupinga na kubeza juhudi kubwa za serikali zenye kuleta mabadiliko kimaendeleo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli huku wengi wao wakitaka kutikisa mshikamano wa chama hicho.

Alisema watu hao hawatabaki salama kwa kuwa lengo lao ni kutaka kuibomoa serikali badala ya kujenga mshikamano utakaoleta maendeleo na amani nchini.

"Wapo ambao wanajifanya vipofu kwamba hawaoni juhudi zilizofanywa na Rais Magufuli. Mimi nawaambia ukiona mtu anapinga kama sio chizi atakuwa ni mkimbizi", alisema Kheri.

Alitumia fursa hiyo kuwataka vijana wa chama hicho wenye sifa, kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali kuanzia serikali za mitaa ili waweze kutumikia wananchi katika maeneo yao.

Aliongeza kuwa vijana ni nguzo kubwa hivyo wazee waliopitia ngazi mbali mbali za uongozi wawasisitize vijana wanaotafuta uongozi kuwa waadilifu ili kuendelea kukijenga chama hicho.

Aidha mwenyekiti huyo aliendesha harambee na kupata shilingi milioni kumi zitakazotumika katika kuboresha jengo la mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti huku akimpongeza mkuu huyo wa mkoa kwa maendeleo yaliyoko katika mkoa huo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utelekezaji wa Umoja wa Vijana Taifa  Bi Joan Kataraia alitoa bendera 400 kwa chama hicho ili kuleta hamasa kwa vijana na ndani ya chama hicho ambapo jumla ya vijana 5 kutoka katika kata ya Hamgembe mtaa wa Kashabo wamerudisha kadi zao toka vyama tofauti tofauti na kijiunga na chama hicho.
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Bukoba

Mjumbe wa Kamati ya Utelekezaji wa Umoja wa Vijana Taifa  Bi Joan Kataraia akizungumza

Mjumbe wa Kamati ya Utelekezaji wa Umoja wa Vijana Taifa  Bi Joan Kataraia akikabidhi bendera 400.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger