Wednesday 31 July 2019

MGEJA AMUOMBA WAZIRI MKUU KUITISHA MKUTANO WA WADAU WA MICHEZO NCHINI

...

 Mwenyekiti mstaafu wa chama cha soka mkoani  Shinyanga  (SHIREFA)  Khamis Mgeja  ambaye pia ni mdau mkubwa wa soka nchini amemuomba  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa kuitisha Mkutano wa wadau wa sekta ya michezo nchini ili  kujadili changamoto na mstakabali wa maendeleo ya michezo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa na watu walio wengi.


Mgeja ambaye pia Kada wa Chama Cha Mapinduzi ambaye kwa sasa amejikita katika sekta ya michezo hususani ile ya kukuza vipaji kwa  Vijana waliopo Wilayani Kahama ameamua kumuomba Waziri Mkuu akiamini ni msikivu na Mwanamichezo mzuri na kuongeza kuwa kama itampendeza  na atakavyoona inafaa, afanye na yeye kuwaita wadau wa sekta ya michezo kama alivyofanya kazi nzuri Dkt. John Pombe Magufuli alipowaita na kukutana na wadau wa sekta nyingine hapa nchini.

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari leo Julai 31,2019 Mjini Kahama na kuhusu mustakabali wa soka letu la Tanzania hususani katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ambayo timu yetu ya taifa imeshiriki kuanzia ile ya chini ya miaka 17 pamoja na ile ya wakubwa ya kombe la mataifa ya Afrika sambamba na michuano hii ya kombe la Mataifa ya Afrika  kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Alisema Michezo kwa sasa ndiyo inachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi pamoja na kuoa ajira kwa makundi makubwa ya Vijana ambao kwa sasa ndio makundi makubwa ambayo yapo mitaani hayana ajira za kudumu na kupitia michezo wanaweza kujiajiri na kujipatia fedha zitakazokuza maisha yao ya kila siku.

Mgeja alisema kuwa katika siku za hivi karibuni Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliitisha Mikutano kwa nyakati tofauti zikiwahusisha wadau kama vile  wa madini na baadae wafanyabiashara, vikao hivyo tuliona vilikuwa na tija mafanikio makubwa katika ujenzi wa Taifa. Baada ya wadau kupata nafasi ya kusema changamoto na mafanikio.

Aidha alisema mkutano huo wa sekta ya michezo kama utaitishwa utatoa fursa ya wadau mbalimbali kutoa michango yao ya kimawazo na  kujadili jinsi gani tutoke hapa tulipo kwenye aibu za mara kwa mara ili twende na kufika kwenye faraja hali ambayo tutapata wadau wengi na ikiwezekana wakawa na mawazo  mazuri tofauti tofauti tukabadilishana mawazo na uzoefu na kufikia muafaka na kupanda daraja la michezo.

Hata hivyo  Mgeja aliwaomba Watanzania hasa  wadau wa michezo wavute subira pamoja na kwamba tumeumia sana na tunaendelea kuumia baada ya matokeo ya mashindano ya watoto chini ya umri wa miaka 17 Afcon yaliyofanyika nchini kwetu na baadae Afcon ya wakubwa Misri hatuna sababu ya kutafuta mchawi wala kumtoa mtu kafara haitatusaidia chochote kuleta mabadiliko ya michezo na kama hatutajielekeza kuwekeza katika michezo Tanzania tutaendelea kuwa washiriki na wala shio washindani na tusitarajie kuvuna bila kupanda kama matunda pori.

Mwenyekiti huyo Mstaafu wa Chama cha soka Mkoani Shinyanga alisema kuwa hakuna njia ya mkato katika mafanikio yoyote yale bila kuwekeza tatizo letu sie watanzania tunataka matokeo mazuri kitu ambacho hakiwezekani hata ukitaka pepo lazima ufe kwanza.

“Msitake pepo bila kufa na inasikitisha tunataka maendeleo bila kuwekeza katika shule za mpira za watoto wadogo hapa nchini na hakuna njia nyingine yeyote ya kupata mafanikiom katika soka bila ya kuwea na shule za kufundisha watoto tangu wakiwa wadogo mapka wanapokuwea wakubwa na kusajiliwa na vilabu vingine”,alisema Mgeja.

Mgeja pia amewapongeza wachezaji na kocha wao Amunike kwa pale walipofikia ni kweli vijana wetu uwezo wao ndipo ulipofikia katika mashindano ya Afcon na Misri ukweli utabaki pale pale. Ni kujidanganya kuwa tungeweza kufika kwenye  robo fainali au nusu fainali na hatimaye fainali hayo yangekuwa maajabu makubwa ya dunia .

Alisema tumejifunza kuanzia Afcon ya watoto na wakubwa Misri tumeona wenzetu Nchi zingine walivyowekeza kwa kiwango cha juu sana katika Academy Nchi kama Madagasca  na Burundi na mfano wa kuigwa na sisi tujipange upya naimani tutafika pazuri penye faraja na sasa tumeingia katika mashindano ya Afcon ya wachezaji wa ndani na watanzania wanapenda kuona mabadiliko makubwa katika soka letu.

Alisema kuwa michezo kwa sasa hapa Duniani ndio chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kujenga afya za mwili na kama serikali itaongea na wadau mbalimbali kama ilivyo kwa sekta nyingine kunaweza kukaleta mabadiliko makubwa na hivyo kufanya nchi yetu kukua kwa kiwango cha juu katika sekta ya michezi kama ilivyo kwa nchini nyingine barani Afrika.

Mgeja pia aliwapongeza ushirikiano mkubwa kama Taifa ulivyooneshwa katika mashindano ya Afcon chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika Nchini na Afcon ya wakubwa tuliyoshiriki Misri, Ushirikiano wa pamoja wa hali na mali ukiongonzwa na Mhe Rais Dr. John  Magufuli, Makamu wa Rais ,Waziri mkuu, Waziri wa michezo viongozi wa TFF, Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji Taifa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Wadhamini mbalimbali wasani na Watanzania wote  kwa ushirikiano huu tuliouonesha tunaweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio kama walivyofanya nchi zingine Mfano Aljeria, Everycost, Cameroon, Nigeria, Misri, Tunisia na Senegal.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger