Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila
Na Lydia Lugakila - Malunde1 blog Bukoba
Mkuu wa wilaya ya Missenyi mkoani Kagera Kanali Denice Mwila amewataka wananchi wilayani Missenyi kuacha tabia za kuwapokea na kuwahifadhi wahamiaji haramu kutoka nchi jirani kwani tabia hizo zinaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Akizungumza na Malunde 1 blog leo Julai 31,2019 Kanali Mwila ametoa amesema vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha wahamiaji haramu kuongezeka wilayani missenyi mkoani hapa hivyo kupelekea watanzania kukosa ardhi ya kulima na kufanya shughuli za ufugaji.
Kanali Mwila amewataka Watanzania katika maeneo ya mipakani hususani kata za Mtukula,Kakunyu na Minziro waepuke kupokea rushwa kutoka kwa wahamiaji ili wawape hifadhi.
Ameonya kuwa serikali wilayani humo haitawafumbia macho wananchi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.
0 comments:
Post a Comment