Mwenyekiti wa shirikisho la tiba asili mkoa wa Iringa ,Abdu Kisige amesema hawaunga mkono tamko la waganga wa jadi kutoka kijiji cha Gamboshi na wilaya ya Bariadi mkoani Simiyukutoa onyo kali kuwa watampoteza mwanachama yeyote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), atakayethubutu kuchukua fomu ya kugombea urais mwaka 2020 na kumpinga Rais John Magufuli.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi mkoani Simiyu,Bwimila Shala alisema waganga wa jadi mkoani humo watahakikisha kuwa mwaka huu na mwaka unaokuja kwenye uchaguzi wanamlinda na yeyote yule atakayechukua fomu bila utaratibu wa waganga wa tiba asili watampoteza kwa njia yoyote ile.
Hata hivyo,Mwenyekiti wa shirikisho la tiba asili mkoa wa Iringa ,Abdu Kisige (pichani) leo amesema tamko hilo la waganga wa jadi kutoka Simiyu ni kinyume cha demokrasia.
"Waganga wa jadi Simiyu ni mashabiki wasiokuwa na demokrasia,wao wanatafuta tu wapendezwe,wanataka tu wapate sifa kwa rais,lakini ukweli hiyo siyo demokrasia na wala rais hawezi hayo kupendezwa nayo wala sisi watu wa Iringa hatukubaliani na hilo,sisi tunasema demokrasia ifanyike,anayetaka urais agombee,tatizo watu wengi wanashindwa kujua maana ya demokrasia,maana ya demokrasia siyo kulazimisha kila mtu atoe wazo lake", - Kisige
MTAZAME HAPA AKIZUNGUMZA
MTAZAME HAPA AKIZUNGUMZA
0 comments:
Post a Comment