Wednesday 31 July 2019

Ombi la Rais Magufuli kwa kampuni ya ujenzi Njombe latekelezwa

...
Na.Amiri kilagalila-Njombe
Kampuni ya ujenzi wa barabara ya kichina China Henan international cooperation group co ltd (CHICO) inayotekeleza mradi wa barabara wa km 53.9 Njombe-Moronga kuelekea wilayani Makete mkoani Njombe.

Imeanza utekelezaji wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na bwalo moja la chakula katika shule ya msingi ramadhani mjini Njombe kutokana na ombi la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliloomba wakati wa ziara yake april 10 mkoani hapo mara baada ya Rais Magufuli kuombwa na wanafunzi wa shule hiyo wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya  Njombe-Makete.

Waziri wa ujenzi Elias kwandikwa amefika na kukagua shughuli zinazoendelea katika ujenzi huo na kumshukuru mkandarasi kwa utekelezaji huo.

“Kwanza nimshukuru sana mheshimiwa Rais alivyoweza kulisukuma jambo hili na hatimaye tumepata huu mradi  lakini pia na hawa wenzetu wa Chico kwa haraka wameanza utekelezaji kwa kweli mimi ninashukuru sana”alisema Kwandikwa

Lusekelo kijalo ni injinia wa kampuni hiyo amesema ujenzi wa majengo hayo unategemewa kukamilika kabla ya mwezi mmoja na nusu kuisha huku ujenzi huo ukigharimu karibu milioni 240 pindi utakapokamilika

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Ephrahim sanga amesema mradi huo ni mkubwa katika shule hiyo kwa kuwa ina wanafunzi 1552 na kupelekea kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

“Mimi hapa nina wanafunzi 1552 wavulana 648 na wasichana 604 vyumba vyetu vya madarasa ni vichache sana havitoshelezi,ingawa tulikuwa na mpango wa kujenga shule nyingine mpya lakini mh.Rais ametutangulia kwa kweli tunashukuru tukaona tuanzie hapa ili tuweze kuigawa shule pawe na mikondo miwili”amesema mwl.Sanga


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger