Sunday 21 July 2019

KATIBU MWENEZI WA CHADEMA AKUTWA AMEJINYONGA KWENYE MTI

...

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika kata ya Igurwa wilayani Karagwe mkoani Kagera Nurubet Bakaishumba (35) amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani huku sababu za kujinyonga zikiwa hazijafahamika.

Akizungumza katika eneo la tukio diwani wa kata ya Igurwa Wilbad Abdala amesema katibu huyo Nurubet Bakaishumba (35)ambaye pia alikuwa mjumbe katika serikali ya kijiji cha Bwera amekutwa amejinyonga kwenye mti jirani na nyumba yake.

Amesemamwili wa marehemu umegunduliwa na baadhi ya wanakijiji Julai 20,2019 huku akiacha ujumbe wa maandishi unaoeleza kuwa familia yake haihusiki na kifo chake na kumtaka mke wake atunze watoto aliowaacha na kuonesha mali zake zilipo.

Abdala amesema kuwa ujumbe huo aliouacha marehemu amesema kuwa uamzi huo wa kujinyonga ni wa kwake mwenyewe na kwamba wazo hilo alikuwa nalo kwa muda wa mwezi mmoja.

Katibu wa Chadema wilaya ya Karagwe Amoni Minyango amesema chama hicho kimepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika maendeleo ya chama hicho ulikuwa mkubwa.
Tutawaletea taarifa zaidi hivi punde
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger