Monday, 14 January 2019

WAKAZI WA MADALE NA VITONGOJI VYAKE KUFURAHIA HUDUMA YA MAJI DAWASA

...

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wakati alipotembelea Tenki la maji la Wazo na kuwahakikishia Watapata maji kama walivyoahidiwa na Afisa Mtendaji wa DAWASA. Picha zote na Cathbert Kajunason/MMG.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza mbele ya wananchi wa Tegeta Wazo na kuwahakikishia maji safi na salama kufikia leo usiku.
Mmoja ya wananchi akitoa shukrani mara baada ya kumaliza mkutano.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (wa pili toka kushoto) akiw ana wananchi wakikagua maji yaliyokuwa yakitolewa katika tanki la maji ili kuweza maji safi tayari kuwasambazia wananchi.
Pampu za maji zilizofungwa ili kuweza kuwasambazia wananchi maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakishuka kutoka katika tanki la maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakikagua umaliziaji wa bomba ili kuweza kuwapatia maji wakazi wa Kata ya Madale na vitongoji vyake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati alipotembelea tenki la maji la Wazo.


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imewahakikishia wananchi wa Kata ya Wazo kupata maji kwa kipindi chote kwa mwaka mzima bila kukatika. 

DAWASA imewekeza zaidi kwa kujenga tanki kubwa litakalokuwa likizalisha lita milioni sita tofauti na mwanzo ilipokuwa ikizalisha lita elfu sitini tu kwa mwaka.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja mbele ya wananchi akiwemo Mkuu wa Wilaya Kinondoni Daniel Chongolo, wakati akifafanua jinsi ya kutatua changamoto ya maji iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa Kata ya Wazo na vitongoji vyake.

Amesema kuwa kulikuwa na changamoto kidogo ila kwa sasa wananchi wote waliokuwa kwenye mtandao wa maji wa zamani wataanza kupata maji kuanzia saa 2 usiku.

"Naomba niwatoe wasiwasi wananchi maana mradi huu wa sasa una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni sita kwa sasa tofauti na ule wa zamani uliokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita elfu sitini na kupelekea mgao wa maji kwenye maeneo mengi," amesema Luhemeja.

Ameonheza kuwa kuanzia sasa hakutakuwa na mgao wa maji kwenye maeneo yote yaliyo na mtandao wa maji wamejipanga kuwahudumia ipasavyo wakazi hao.

Akielezea maeneo ambayo hayajafika mradi kutokana na kutokuwepo kwa mtandao wa 

maji, Mhandisi Luhemeja amesema kuna fedha takribani Bilioni 115 zimeshapatikana kwa ajili ya kusambaza mabomba yenye urefu wa Kilometa zaidi ya 1000 katika maeneo yote ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Kuna shilingi bilioni 115 zimeshatengwa tayari na zipo kwenye mchakato wa mwisho ili ziweze kutoka tuweze kuwahudumia wale wote ambao hawajafikiwa na mtandao wa maji kwa jiji la Dar es Salaam na Pwani,”amesema Luhemeja.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Mh.Daniel Chongolo amesema katika serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli miradi mingi imekuwa ikitekelezwa na wananchi wawe na subira na wameshaahidiwa maji kutoka kuanzia usiku wa leo.

Chongolo amesema, yeye binafsi anaamini kuwa Mtendaji Mkuu wa DAWASA sio mwanasiasa hawezi kudanganya kazi imefanyika na inaonekana ya kutoka uzalishaji wa maji lita elfu sita hadi milioni sita kwa lisaa.

"Kiukweli siwezi kuwasema vibaya DAWASA maana wamekuwa wakitoa huduma nzuri na hawa ni watendaji wala si wanasiasa hawawezi kuwaongopea, niwaombe tu wananchi muendelee kuwa wapole na wavumilivu wakati wanaendelea kuwatatulia matatizo yenu ya maji, binafsi nitakuja kujionea kwa macho kama maji yameanza kutoka kuanzia Jumannee Januari 15, 2019," amesema Chongolo. 

DAWASA wamedhamiria kufika asilimia 95 ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kufikia Desemba mwaka huu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger