Thursday, 24 January 2019

URAIS WA TUNDU LISSU WAMVURUGA MBUNGE CCM

...
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amefunguka juu ya kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa akipewa nafasi ya kugombea Urais yuko tayari kukiwakilisha chama chake na kudai suala hilo lilikuwa ni ndoto yake.

Musukuma amedai kauli ya Tundu Lissu inaonesha alikuwa akitamani kuwania nafasi ya Urais kwa muda mrefu ndiyo maana amekuwa haonekani mara kwa mara kwenye jimbo lake bali anafanya siasa za kitaifa.

Musukuma amesema, "ukiona mtu aliyenusurika kufa halafu ameamka tu anawaza Urais maana yake alikuwa na ndoto ya kuwa rais wa Tanzania ndiyo maana alipotoka tu kwenye matibabu akasema anataka kuwa Rais wa nchi."

"Tumuombe Mungu kwa kuwa tu amelitanguliza suala la mapenzi ya jinsia moja hata huko kwenye chama chake naamini kuna watu hawataki ushoga kama tumekaa miaka yote bila kupitisha ushoga kwanini tupitishe ushoga kwenye Urais wa Tundu Lissu", ameongeza Musukuma.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa sasa yuko nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu kufuatiwa kushambuliwa kwa risasi mwishoni mwa mwaka 2017 na hivi karibuni baada ya kupata nafuu alitangaza nia ya kuwania Urais endapo ataaminiwa na chama chake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger