Wednesday 16 January 2019

TFF KUBURUZWA MAHAKAMANI SHINYANGA SAKATA LA UCHAGUZI WA VIONGOZI YANGA

...
Mwanachama wa Yanga Chibura Makorongo mkazi wa wilaya na mkoa wa Shinyanga mwenye kadi ya uanachama wa Yanga namba 0015249 amehitaji ufafanuzi kutoka kwa kamati ya shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) inayosimamia uchaguzi wa viongozi wa Yanga, kuhusu tafsiri ya uhalali wa uanachama wa Yanga kupitia Benki ya Posta, pia suala la viongozi wa klabu hiyo kuikacha mikoa mingine kuomba kura za kuiongoza klabu hiyo. 

Chibura amesema hayo wakati akizungumza na www.malunde.com kuhusu sintofahamu ya mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa klabu ya Yanga na kusema kuwa endapo mambo hayo hayatatolewa ufafanuzi yupo tayari kwenda mahakamani kusitisha zoezi la uchaguzi ambalo linasimamiwa na shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF). 

“Wanachama wa Yanga waliopitia mfumo wa kujiunga kupitia Benki ya Posta ni wanachama halali au la! Na kama ni la! Ni nani aliyepitisha suala hilo?” Aliuliza Chibura. 

“Na hao viongozi wanaowania nafasi mbona wameitenga mikoa mingine? Wakipata dhamana ya uongozi watakuwa wanawaongoza wanachama wa Dar es salaam ama wanachama wa nchi nzima? Tunapokwenda kwenye uchaguzi tutakwenda mahakamani hasa mimi nimeshaanza kuwasiliana na mwanasheria wangu,” Aliongeza Chibura.

Klabu ya Yanga licha ya kukabiliwa na misukosuko ya makundi mawili yanayosigana lakini klabu hiyo inakalia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa na alama 53,ikiwa imecheza mechi 19 bila ya kupoteza mchezo hata mmoja,ikifuatiwa na timu ya Azam fc yenye alama 40 baada ya kucheza michezo 17,huku Simba Sc ikishikilia nafasi ya tatu ikiwa na alama 33 baada ya kuchez mechi 14.


Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger