Tuesday, 1 January 2019

SALAH,MANE NA AUBAMEYANG KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA - CAF

...

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, Sadio Mane na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Merick Aubameyang ndiyo wachezaji watatu wa mwisho wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Orodha hiyo ni marudio ya wachezaji watatu waliotajwa kuwania tuzo ya msimu uliopita, ambapo itatolewa kwa kuzingatia kiwango cha mchezaji husika katika mwaka 2018.

Pierre-Merick Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon, amefanikiwa kuwepo katika listi ya mwisho ya wachezaji watatu wa tuzo hizo kwa mara ya tano mfululizo sasa tangu mwaka 2014 na kuifikia rekodi ya mkongwe wa Ivory Coast, Yaya Toure na wa Ghana, Michael Essien.

Mohamed Salah ambaye aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kushinda tuzo hiyo tangu ilipoasisiwa mwaka 1992. Ametajwa katika listi ya wachezaji watatu wa mwisho kwa miaka miwili mfululizo huku akishinda kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

Kwa upande wa Sadio Mane, ametajwa katika listi ya wachezaji watatu wa mwisho wa tuzo hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku akiwa hajashinda tuzo hiyo mpaka sasa.

Kilele cha tuzo hizo kinatarajiwa kufanyika Januari 8, 2019 mjini Dakar, Senegal.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger