Morogoro Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro kimesema vyama vya siasa katika mataifa yalioendelea havifanyi mikutano ya hadhara wala maandamano bila vibali mara baada ya chaguzi kuu kumalizika lakini inashashangaza mikutano hiyo ikishinikizwa ifanyike Barani Afrika. Kimeeleza maendeleo yaliopatikana Marekani na ulaya yangekawia mno iwapo wananchi wake wangepuuzia kazi za uzalishaji mali,kujiendeleza kielimu na kundekeza siasa kama inavyotakiwa ifanyike katika nchi za ulimwengu wa tatu . Msimamo huo ulitolewa jana na katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka,kwa nyakati tofauti akiwa ameambatana na secretarieti ya CCM mkoa wa…
0 comments:
Post a Comment