Wednesday, 2 January 2019

Picha: MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA AWAPONGEZA WALIOSHIRIKI MICHUANO YA UVCCM CUP SHINYANGA

...

Chama cha mapinduzi CCM kata ya Kambarage Mjini Shinyanga kimefanya sherehe ya kuzipongeza timu za vijana za mpira wa miguu, zilizoshiriki katika mashindano ya ya Kombe la Vijana (UVCCM CUP) Wilaya ya Shinyanga 

Sherehe hiyo imefanyika Jumanne , Januari 1, 2019 katika ukumbi wa Shy Villa uliopo kambarage Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Mh.Stephen Masele. 

Akizungumza wakati wa sherehe hizo Mh. Masele amewapongeza vijana walioshiriki katika michuano ya kombe la Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) huku akiwataka kuongeza bidii zaidi katika soka ili waweze kuonekana na vilabu vikubwa . 

‘Endeleeni kushirikiana maana mpira wa miguu ni kama siasa ni kazi ya kitimu kwenye siasa huwezi fanikiwa peke yako lazima uende na wenzako, kwa hiyo mkijitahidi hata timu yetu ya stand lazima iweke jicho lake kuangalia wachezaji wa nyumbani’alisema Masele. 

Katika hatua nyingine Mh. Masele amewakumbusha UVCCM kupuuzia maneno ya watu yenye lengo la kuwakatisha tamaa na badala yake waongeze ushirikaiano zaidi katika kufanya kazi . 

‘Msiwe na wasiwasi maneno haya yapo tu siku zote kwa hiyo fanyeni kazi simamie misingi ya chama , ukisikia maneno na ukaendelea kufanya kazi ndio kukomaa huko’ alisema Masele. 

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kambarage Hasan Mwendapole amesema kuwa lengo la kufanya sherehe hiyo ni kuwakutanisha vijana wote walioshiriki katika mashindano hayo ili kujenga umoja na mshikamano ambao utakuwa chachu ya maendeleo katika wilaya ya Shinyanga. 

‘Haya mashindano yamechezwa karibu wiki tatu , kila siku vijana walikuwa wanakutana kwa hiyo unakuwa umewaweka pamoja hata muda wa kutembea hovyo haukuwepo’ alisema Mwendapole 

Mashindano ya kombe la umoja wa vijana wa CCM (UVCCM CUP) yalijumuisha kata zote za Wilaya ya Shinyanga na aliyeibuka kidedea ni timu ya Kata ya Kambarage na kukabidhiwa Ngao, cheti pamoja na Ng’ombe.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakary Mkadam (kushoto) akiteta jambo na Mh. Stephen Masele
Diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akisisitiza jambo wakati wa sherehe hizo ambapo amewataka vijana kuendeleza ushirikiano katika michezo ili kuwa chachu ya mendeleo . 
Mwenyekiti wa mashindano hayo BI. Jackline Chacha Amesema lengo la mashindano hayo ni kutekeleza ilani ya chama ,huku akiweka wazi kuwa wameunda timu ya wilaya itakayowahusisha vijana kutoka katika timu zilizoshiriki.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Comrade Egobano akisisitiza jambo katika Sherehe hiyo
Andrew Manyonyi Kampteni  wa timu ya Kata ya Kambarage amewaomba wadau wa soka mkoani Shinyanga  kujitokeza kusapoti timu za vijana kwani wanakumbana na changamoto mbalimbali hasa upande wa vifaa vya michezo.

Mbunge wa Shinyanga Mjini Mh. Masele akipokea hati ya pongezi kutokana na mchango wake ndani ya Chama CCM Wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi akipokea hati ya pongezi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Masele
Mh. Stephen Masele akimkabidhi Comrade Egobano (kushoto)  cheti cha pongezi kutokana na mchango wake kwa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Wilaya ya Shinyanga.
Mh.Stephen  Masele akikata Keki katika Sherehe hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Abubakary Mkadam na kushoto ni Mwenyekiti CCM kata ya Kambarage Rehema Nhamanilo.

Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Kambarage wakiwa eneo la Sherehe wakifuatilia yanayojiri.
Wadau  wa michezo pamoja na wanachama wa CCM wakifuatilia kwa makini kinachoendelea katika Sherehe hizo.
Sherehe inaendelea


.
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika  na Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa michuano ya UVCCM CUP Wilaya ya Shinyanga  timu kutoka Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.
Picha na Steve Kanyefu- Malunde1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger