Mchezaji Sala ambaye alikuwa kwenye ndege hiyo.
Mshambuliaji mpya wa klabu ya Cardiff City Emiliano Sala, amepotea angani kwenye ndege binafsi jana jumatatu jioni wakati anatoka mjini Nantes, Ufaransa kuelekea Cardiff, Wales.
Mamlaka ya anga ya Ufaransa imethibitisha ndege hiyo kupotea ambapo muargentina huyo mwenye miaka 28 alikuwepo pamoja na mtu mwingine wa pili.
Sala alisajiliwa kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 15 siku ya Jumamosi na alikuwa ni miongoni mwa watu wawili waliokuwepo kwenye ndege hiyo iliyopotea.
Baada ya kusaini mkataba siku ya Jumamosi, Sala alirejea nchini Ufaransa kuwaaga wachezaji wa timu yake ya zamani ya Nantes, na baadaye kuweka picha akiwa na wachezaji hao katika Instagram akiandika “ Kwa heri ya mwisho “ kabla ya kupanda ndege kurejea Wales.
Afisa anayehusika katika kuitafuta ndege hiyo John Fitzgerald anasema kuwa hatarajii kumkuta mtu yoyote akiwa hai.
“Kuna bahati ya asilimia 5 tu ya kuwapata Sala na rubani, “alisema Fitzgerald.‘ Maji ni ya baridi sana kwa sasa , kwa hiyo kama kuna ambaye amepona kwenye maji , ni baridi sana , ni saa moja tu unaweza kuwa mzima katika kipindi hiki cha mwaka‘ .
Familia ya mchezaji huyo ipo nchini Argentina na baba wa mchezaji huyo Horacio amesema alijisikia vibaya sana baada ya kupata taarifa za kupotea kwa mwanae.
0 comments:
Post a Comment