Mwanafunzi wa chuo cha St. John nchini Zimbabwe ameupeleka uongozi wa chuo hicho mahakamani, baada ya kuzuiwa kuingia chuoni kwa kosa la kufuga ndevu.
Baba wa mtoto huyo Bw. Mohammed Ismail, amefungua shtaka rasmi kwa niaba ya mtoto wake kwenye Mahakama Kuu ya nchi hiyo, akidai kwamba kitendo hicho ni kuvunja katiba ya nchi na unyanyasaji.
Akiendelea kuelezea tukio hilo, Bw. Mohamed amesema kwamba mtoto wake huyo amekuwa akirudishwa mara kwa mara na uongozi wa chuo, ili anyoe nywele wakidai kuwa anakiuka sheria za chuo.
Baba huyo amesema kwamba suala hilo linaruhusiwa kwa mujibu wa dini yao ya Kiislam na kwamba mtoto wake alikuwa anasoma ili aje kuwa 'Imam', lakini uongozi wa chuo hauruhusu suala hilo, jambo ambalo limekuwa likimpa shida mwanafunzi huyo kwa kurudishwa nyumbani mara kwa mara.
Hata hivyo Mahakama ya nchi hiyo bado haijataja tarehe ya kusikiliza kesi hiyo.
0 comments:
Post a Comment