Monday, 14 January 2019

MAKOCHA WAPYA WA SINGIDA UNITED WAANZA KUCHAPA KAZI

...

Kikosi cha Singida United

Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kuwa makocha wao wapya wamewasili jijini Mwanza na kuungana na timu tayari kuanza kazi ya kusaka alama tatu dhidi ya Mbao FC.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga ameiambia www.eatv.tv kuwa benchi lao hilo jipya la ufundi limechukua majukumu tayari kutoka kwa makocha waliokuwa na timu.

''Makocha wetu wameshaungana na timu Mwanza, tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao FC siku ya Jumatano, makocha hao ni kocha mkuu Dragan Popadic, kocha msaidizi Dusan Kondic na wataendelea na kocha wa makipa Mirambo'', amesema Sanga.

Makocha wapya wa Singida United.

Aliyekuwa kocha mkuu wa Singida United, Hemed Morocco amepewa majukumu katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys. Makocha wengine Jabir Mahamoud na Shadrack Sanjigwa wataendelea na kikosi B cha timu hiyo.

Singida United ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya tano, kwasasa ipo katika nafasi ya 10 wakiwa na alama 24 katika mechi 20 walizocheza.
Via>> EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger