Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) amejiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally.
Otto amejiunga CCM leo Jumatatu Januari 7,2019 wakati wa mkutano wa Katibu huyo wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kadi ya CUF na busara tano za kustawisha Chama cha Mapunduzi,Otto alisema ameamua kujiunga CCM kwa sababu ni chama chenye mipango kazi inayotekelezwa kwa vitendo na uaminifu kama mwenye Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015.
“Nimeamua kujiunga CCM kwa sababu ya utashi nilionao wa kutumikia wananchi kupitia siasa na kuamini kwamba CCM ndiyo mahali pekee penye ndoto na dira ya utekelezaji wa sera ili kuwaletea maendeleo wananchi”,alisema Otto.
“Mheshimiwa Katibu Mkuu,naomba kukukabidhi bango langu nililolitumia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 nikiwania ubunge jimbo la Kwimba lakini pia naomba kukukabidhi karatasi hii yenye busara tano zinazolenga kukistawisha Chama Cha Mapinduzi”,aliongeza.
Akiwa katika mkutano huo,Katibu Mkuu wa CCM ,Dkt. Bashiru Ally amepokea wanachama 126 wapya wakiwemo kutoka vyama vya upinzani.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akizungumza wakati wa kujiunga CCM leo -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Katibu mkuu CCM ,Dkt. Bashiru Ally akiwa ameshikilia bango la Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA).Kulia ni Ntiga Julius Otto akiwa ameshikilia karatasi yenye busara tano za kustawisha Chama Cha Mapinduzi aliyoikabidhi kwa Dkt. Bashiru.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akishikana mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akimkaribisha CCM.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akiwa amekaa na makada wenzake wa CCM katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment