Wednesday, 9 January 2019

KESI YA KUONGEA HOVYO HOVYO INAYOMKABILI HALIMA MDEE YAPIGWA KALENDA

...
Kesi inayomkabili, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee anayekabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusikilizwa Februari 7, 2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 mbele ya hakimu mkazi mkuu Salum Ally kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea na ushahidi lakini hakimu husika yuko likizo.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini kutokana na hakimu husika kuwa likizo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi," amedai Wakili Mwita.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 7, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na hatua ya ushahidi. Tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.

Katika kesi hiyo, Halima anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 4, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Mdee anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kwa kusema “anaongea hovyo hovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger