Wednesday, 2 January 2019

KESI YA JAMAL MALINZI NA WENZAKE KUSIKILIZWA SIKU TATU MFULULIZO

...
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza ushahidi wa kesi ya Utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF) Jamal Malinzi na wenzake kwa siku tatu mfululizo.

Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuitishwa leo kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo iliyofikia shahidi wa 10, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 16, 17 na 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Malinzi na wenzake waliwatakiwa kheri ya mwaka mpya, ndugu, jamaa na rafiki waliofika katika kesi yao.

Washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wakikabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger