HUKU mashabiki wa Yanga wakiiona timu yao haina fedha na masikini kumbe wanajidanganya baada ya kocha mkuu wao kipenzi, Mwinyi Zahera, kutamka wazi kwamba anaweza kuifanya klabu hiyo kumaliza ukata wa kifedha ndani ya miezi miwili kutokana na hazina kubwa ya wanachama na mashabiki iliyonayo. Yanga ni klabu kongwe nchini, lakini imekuwa ikishindwa kutumia rasilimali ilizonazo katika kujiletea maendeleo, huku baadhi ya wadau wakidai tatizo hilo linasababishwa na viongozi wanaojali masilahi yao binafsi na si ya klabu. Pamoja na kuwa na majengo mawili katika ya Jiji la Dar es Salaam,…
0 comments:
Post a Comment