Leo Januari 23, 2019 Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na viongozi mbalimbali wa Dini Ikulu Dar es Salaam na kuongea nao.
Mchungaji Josephat Mwingira alipata nafasi ya kusimama na kuongea mbele ya Rais Magufuli.
“Mipango miji ni ya Mungu, mivurugano ni ya shetani, tuwe na mpango mkakati wa muda mrefu mathalani wa miaka 50 katika Miundombinu ili tusiwavunjie vunjie wananchi nyumba zao kila wakati, tuna Wataalam tuliowasomesha kwa nini hili linaendelea? tuliangalie hili.” Amesema Mchungaji Josephat Mwingira.
Ameendelea kusema; “Suala la Wakuu wa Wilaya kutoa amri ya kuwaweka watu ndani wakiwemo Viongozi wa dini, unamweka Kiongozi ndani hii inanipa shida kidogo, je wanataka tuichukie Serikali yetu? Naomba wakuu hao wasipewe mamlaka hayo, wanaitia aibu Serikali kwa kudhalilisha watu.
“Mimi nina ushahidi, kule Sengerema Mchungaji wangu aliswekwa ndani na Kanisa likabomolewa, sasa nikajiuliza hii maana yake nini? Wakuu wa Wilaya wana madaraka yaliyopitiliza, wanaitia aibu Serikali.”
“Mhe. Rais, samahani kwa kusema umechelewa kidogo kutuita, ninashauri tu kwamba kabla haujazipeleka sera zako, ni vizuri tukae pamoja na kujadili kwa sababu ukiwa peke yako inakuwa vigumu sana.” Amemalizia kusema Mch. Josephat Mwingira.
0 comments:
Post a Comment