Mgomo huo ulioanza saa nne usiku jana kwa waafunzi zaidi ya 1,000 kutoka mabwenini na kukusanyika katika eneo la migomo linalojulikana kama Block G, Mabibo unatarajia kuendelea tena asubuhi ya leo katika eneo la Revolution Square, Main Campus.
Mgomo huo unafanyika huku wanafunzi hao wakiwa na hoja kuu nne dhidi ya Serikali ya Tanzania.
Hoja hizo ni kama ifuatavyo;
1. Wanahitaji kuongezwa kwa majina ya mikopo ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza, kwani mpaka sasa wanafunzi wa UDSM mwaka wa kwanza waliopewa mikopo ni 3,996 tu kati ya 8,321.
2. Wanashinikiza serikali kuwapa mikopo wanafunzi wote yatima na wanaosoma masomo yaliyotajwa kama ni vipaumbele vya taifa ikiwemo uhandisi na sayansi. Licha ya serikali kutangaza kuwa yatima, walemavu na wanaosoma uhandisi na Sayansi watapewa kipaumbele katika mikopo lakini wanafunzi wengi wenye sifa hizo wamenyima mikopo.
3. Wanafunzi wote ambao wamepata mikopo wanaitaka serikali iwapatie Fedha zao za kujikimu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kwani ni wiki tatu sasa tangu wafungue Chuo kuanza masomo lakini hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepewa fedha ya kujikimu jambo ambalo limesababisha njaa kali kwa wanafunzi na hata wengine kushindwa kuhudhuria vipindi na kuishia kulala mabwenini wakila mikate ambapo Cafeteria za Chuo zimebaki tupu zikiwa na wateja wachache.
4. Wanaitaka serikali iamuru kuondolewa kwa tozo ya kinyonyaji ya Sh. 20,000/= kila mwaka kwa kila mwanafunzi wa Chuo kikuu Tanzania ili kuchangia uendeshwaji wa TCU.
Tozo hii ni mpya iliyoanzishwa na kupitia tozo hiyo TCU imekuwa ikikusanya Sh. 20,000/= kwa kila mwanafunzi (Jumla inayokaribia Sh. bilioni 4 kwa mwaka) kwa madai kuwa wanafunzi wanatakiwa kuchangia uendeshwaji wa taasisi hiyo ya umma, jambo ambalo halikuwepo miaka ya nyuma.
Wanafunzi wanaona tozo hii ni kubwa na ya kinyonyaji kwani wao wamekuwa wakichangia Sh. 50,000/= TCU kila wanapoomba kudahiliwa, hivyo wameeleza kuwa kuanzishwa kwa mfumo wa kuchangia kila mwaka si sawa.
Updates zaidi zitafuata ikiwo picha, audio na video za mgomo huo asubuhi ya leo tarehe 4 Novemba, 2016.
0 comments:
Post a Comment