Saturday, 4 June 2016

Wasanii wafanya uchafu!

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

wasaniiiiZainabu Ally na Naomy Mmbaga wakifanya yao.
Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Katika hali ya kushangaza, wasanii wa kike wanaochipukia kwenye anga la filamu Bongo, Zainabu Ally na Naomy Mmbaga, wamenaswa wakifanya vitendo vichafu wakiwa lokesheni.
Tukio hilo lililopigwa chabo na kachero wetu, lilijiri juzikati katika Hoteli ya KD iliyopo maeneo ya Akachube, Kijitonyama jijini Dar wakati wasanii hao walipokuwa wakiigiza muvi yao ndipo walipofanya uchafu huo baada ya kukolea na ‘ulabu’.
“Awali kabla ya kuanza kurekodi walianza kupiga mambo yao, baada ya kurekodi ndipo wakaongezea tena mitungi na hapo ndipo walipokolea na kuanza kufanya mambo ya ajabu,” alizungumza kachero wa kujitegemea aliyeshuhudia tukio hilo.
Kachero wetu alifanikiwa kuwafotoa picha kadhaa lakini alipojaribu kuwauliza kulikoni wafanye vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Kitanzania, wasanii hao hawakutoa majibu ya moja kwa moja kutokana na kukolea ulabu.
Hata hivyo, kesho yake Naomy alipatikana na alipoulizwa kwa nini walifanya vitendo hivyo aliomba stori hiyo isitoke kwa madai itamharibia.
“Please iache hiyo bwana, itaniharibia. Si unajua yale ni mambo ya lokesheni tena, mzee akijua itakuwa noma,” alisema Naomy ambaye ameshauza nyago kwenye Sinema ya Laghai, Penzi la Giza, F.B.I, Part of Job Samira na nyingine kibao.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger