Habari zenu,
Wiki iliyopita Serikali kupitia chuo kikuu cha udom,ilitangaza kwamba Wanafunzi wote wanaosoma diploma ya ualimu "special diploma" chuo kikuu cha Udom wanatakiwa warudi nyumbani kutokana na mgomo wa walimu wao kutokuwafundisha tangu tarehe 6.5.2016.
Kutokana na hali hiyo ni kwamba wanafunzi hao waliharibika kiakili na kisaikolojia,na hawajui nini cha kufanya,lakini siku ya jana Mkuu wa nchi JPM alitangaza kwamba,wanafunzi wamerudishwa nyumbani kutokana na kwamba hawana sifa za kujiunga chuoni hapo.
MASWAYETU BLOG tumeona si vyema mkabaki mkiwa nyumbani hamna cha kufanya ,tumeamua kuleta ushauri ambao utawasaidia watu wote walirudishwa nyumbani.
Kutokana na kauli ya JPM ni kwamba wanafunzi hawa hawatarudi chuoni hivyo wakatafute vyuo vya level yao.
nini ufanye?
Naamini una matokeo mazuri ambayo ulifaulu vizuri ya kidato cha nne ,div 1,2,au 3.
Fanya application za vyuo vya AFYA,KILIMO NA MIFUGO,UALIMU na kozi mbalimbali ktk vyuo vyetu vilivyopo hapa Tanzania.
DEADLINE YA KUFANYA APPLICATION NI TAR 3/6/2016,fanya upesi kufanya application NAKUHAKIKISHIA UTAPATA CHUO na UTASOMA.
HII ITAKUEPUSHA KUKAA NYUMBANI MWAKA MZIMA NA KUENDELEA KUPOTEZA MUDA.
CHUKUA HATUA SASA.
0 comments:
Post a Comment