PROFESA LUGHANO J. KUSILUKA ATEULIWA KUWA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU MZUMBE
Hii ni kukufahamisha kwamba, Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Mh. Barnabas A. Sammata (Jaji Mkuu Mstaafu), kwa Mamlaka aliyokabidhiwa na sehemu ya Pili, Kifungu Na. 5(1) cha Hati Ridhia ya Chuo Kikuu Mzumbe, 2007 amemteua PROFESA LUGHANO J. KUSILUKA kuwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe kwa kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016 badi tarehe 2 Juni, 2021.
Wanajumuiya wote mnaombwa kumpa ushirikiano ili kwa pamoja tuweze kufikia misheni ya Chuo kikuu Mzumbe.
0 comments:
Post a Comment