Polisi mkoani Mwanza wamemuua jambazi mmoja baada ya kujibizana kwa risasi mida ya saa 7 ( saba ) usiku
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi ambaye alikuwa
kwenye eneo la tukio, amesema katika tukio hilo, askari mmoja
amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na jambazi huyo aliyeuawa ambaye
alikuwa na mwenzake anayedaiwa kukimbilia kwenye majabali ya mawe.
Amesema majibizano hayo yalianza saa 6.20 katika Mtaa wa Utemini, baada ya polisi waliokuwa doria kufuatilia nyendo za watu hao.
“Tulipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa katika eneo hilo kuna watu wanaowatilia shaka, ndipo askari wakaamua kuwafuatilia. "
Hata hivyo, amesema wamefanikiwa kukamata bastola moja iliyokuwa ikitumiwa na jambazi huyo.
Hata hivyo, amesema wamefanikiwa kukamata bastola moja iliyokuwa ikitumiwa na jambazi huyo.
“Unasikia
milio hiyo ya risasi, askari wanaendelea kumsaka huyo mmoja
aliyejificha kwenye mawe, naimani tutampata tu na hatuondoki hapa mpaka
tumtie mikononi,” alisema Msangi na kuongeza:
“Hawa
ni majambazi sugu ambao walikuwa wakituhumiwa kufanya matukio ya
uporaji na mauaji jijini hapa, tulikuwa tukiwasaka kwa muda mrefu.”
0 comments:
Post a Comment