Wafanyabiashara nchini wameshauriwa kutumia Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kama uwanja wa kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyao.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan jana Jumanne Julai 2, wakati akizindua maonyesho hayo katika viwanja vya Sababa jijini Dar es Salaam, katika maonyesho hayo yaliyobeba kauli mbiu isemayo ‘usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu’.
Mama Samia alisema maonyesho hayo ambayo yamejizolea umaarufu Afrika Mashariki na Kati hutembelewa na watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo yakitumika vizuri ni sehemu sahihi ya wafanyabiashara kupanua wigo wao kibiashara.
Katika hatua nyingine Mama Samia amewataka wakulima kulima mazao kwa wingi kwani Serikali inaendelea kujenga viwanda ambavyo malighafi yake itatoka hapa nchini hususani katika sekta ya kilimo.
0 comments:
Post a Comment