Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Kangi Lugola ameagiza waliokuwa watumishi watatu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kuyarudisha magari aina ya Toyota Land Cruiser wanayoyamiliki kinyume cha sheria.
Waziri Lugola alitoa kauli hiyo Jumanne hii katika kikao chake na viongozi wa ngazi ya juu wa Nida.
Alisema miongoni mwa watumishi wanaomiliki magari hayo ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Nida, Dickson Maimu.
Alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Arnold Kihaule kushughulikia suala hilo hadi ifikapo jana jioni yawe yamerejeshwa katika maegesho ya ofisi za Nida.
Kikao hicho kilifanyika Jijini Dodoma, na kilikuwa kinapokea taarifa ya idadi ya mali za Nida zilizopo na zilizopokelewa na mwenendo wa matumizi yake.
0 comments:
Post a Comment