Thursday, 25 July 2019

Umoja Wa Wanafunzi Vyuo Vikuu Mkoa Wa Dodoma Wamwandikia Waraka Mzito Rais Magufuli

...
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
UMOJA wa vijana wanafunzi wazalendo wa Vyuo vikuu  Mkoa wa Dodoma,  wamemuandikia Walaka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, wakimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Katika walaka huo uliouwasilishwa na msemaji wa umoja huo, ambaye ni Rais ya serikali ya wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Yohana(st John univesity) Jerry Motela kwa mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.
 
Umoja Wa vijana hao wa vyuo vikuu umeeleza kuridhishwa na kazi kubwa anayoifanya Rais Magufuli  hasa katika kusimamia misingi ya uzalendo na kuwaamini vijana na kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi  hivyo ni jambo la kuigwa kwa viongozi wengine watakaofuata nyayo  zake.
 
“Kwanza kabisa tunapenda kukupongeza wewe binafsi na serikali yako ya awamu ya tano kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya katika nchi yetu, dhumuni la tamko hili ni kuunga mkono na kukutia moyo kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya”
 
“Tunapenda kusema kusema sisi kama vijana tunaimani kubwa sana na wewe binafsi pamoja na serikali yako unayoiongoza,  sisi umoja wa wanafunzi wazalendo wa vyuo vikuu vya Dodoma tumeamua kutoa tamko kwa yote uliyotufanyia vijana wa taifa hili kwa kuwachagua katika ngazi mbalimbali” amesema Motela.
 
Wamemuomba Rais kuwapuuza wale wote  ambao wanaonyesha dalili za viashiria vyovyote vya kutaka kukwamisha juhudi zako za kutuletea maendeleo katika nchi yetu.
 
Pia wamempongeza kwa kuboresha miondombinu ya elimu hapa nchini, ikiwamo kukarabati shule kongwe ili kuendana na hali ya sasa, sambamba na kutoa elimu bure kutoka elimu ya msingi hadi sekondari kidato cha nne.
 
Wamempongeza kwa kuongeza wigo udahili wa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini, kitendo kimetoa fulsa kubwa kwa wanafunzi wengi kuweza kujiunga na elimu ya juu.
 
Wamesema wamefurahishwa na suala la kuboresha mikopo suala ambalo hapo mwanzo lilikuwa sugu na kusababisha migomo ya mara kwa mara katika vyuo mbalimbali hapa nchini.
 
“Mh Rais suala ambalo lilikuwa likionekana sugu na kusababisha migomo mingi katika vyuo vikuu vingi hapa nchini ni suala la ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo jambo umelipatia ufumbuzi, na sasa mikopo hiyo inapatikana tena kwa wakati” amesema.
 
Pia wamempongeza kwa kuboresha miondombinu mbali mbali ikiwamo, katika sekta ya Afya, usafiri wa aina zote na hasa kutengeneza reli ya kisasa na kununua ndege nane tena za kisasa na kurahisisha usafiri huo.
 
Nae mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi wakati akipokea walaka huo, ili kumfikishia Rais wa Tanzania, amewapongeza kwa jambo hilo kwa kusema ni  jambo la kizalendo na linatakiwa kuigwa na vijana wengine kwa sababu ni jambo la kizalendo.
 
“Kwanza niwapongeze kwa jambo hili ni jambo la kizalendo na linatakiwa kuigwa na vijana wengine kwa kuonesha uzalendo kwa kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu mzalendo” amesema.
 
Pia amewapongeza kwa kujikita katika kutoa pongezi kwa kazi kubwa inayofanywa na Rais wan chi,  tofauti na wengine ambao wamejikita katika kuwaponda watu wengine na kuwajibu wengine, lakini wao wamejikita kwa  pongezi.
 
Amesema serikali ya awamu hii ipo kazini kwa ajili  ya kutekeleza ilani ambayo ndiyo aliyoiombea kura kwa wananchi, na  suala kubwa kabisa ni la kukomesha suala lamigogoro na migomo iliyokuwa ikitokea mara kwa mara katika vyuo mbali mbali.
 
Pia amewataka wanafunzi hao  kuwa  mfano kwa jamii na kuiongelea vizuri serikali  hii ambayo imejikita katika kkutatua kero za wananchi, na amewataka kutokuishia hapo tu bali  waendee kuwaelimisha vijana na kusambaza  walaka huo na katika mitandao ya kijamii ili kujenga kizazi cha uzalendo.
 
Kwa upande wake mmoja wa waliokuwepo katika maandamano hayo Jamal Adam, ambaye ni spika wa bunge wa chuo cha serikali za mitaa cha Mipango, amesema wameamua kufanya hivyo ili kusherehesha kazi nzuri ambayo inafanywa na Rais dkt John Magufuli ili hata wale ambao hawaoni anayoyafanya nao wajue mambo makubwa yanayofanywa katika nchi yetu.
 
“ Lengo ni kuwaonesha wale ambao hawaoni kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu, na sisi kama vijana lazima tuoneshe uzalendo kwa kusherehesha yale mazuri ambayo yanafanywa na Rais wetu ili na watu wengine wayaone” amesema Adam.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger