Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma[PSSSF] kuanzia Juni 1 hadi Julai 24,2019 umelipa kiinua mgongo kwa wastaafu elfu mbili ,mia sita na hamsini[2,650] huku zikitumika Tsh.Bilioni 122.9 kulipa wastaafu hao.
Hayo yamesemwa Julai 24,2019 jijini Dodoma na Meneja kiongozi ,uhusiano wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma[PSSSF] Bi.Yunis Chiume wakati akitoa taarifa ya Maendeleo ya Mfuko huo kwa vyombo vya habari.
Bi.Chiume amesema kuwa ,PSSSF unaendelea na jukukumu lamsingi la kulipa pensheni kwa wastaafu ambapo pia umelipa pensheni ya Mwezi kwa wastaafu laki moja,ishirini na sita elfu na arobaini na tatu[126,043] na kiasi kilichotumika ni Tsh.Bilioni 92.7.
Aidha,Bi.Chiume amesema idadi ya wastaafu ambao hawajalipwa mafao imepungua kutoka wastaafu 227 Mwezi Mei,2019 na kubaki wastaafu 119 hadi sasa na sababu zinazosababishwa kutolipwa kwa wastaafu hao ni pamoja na kukosa kwa viambatanisho ,pingamizi la waajiri juu ya vyeti feki,kupokea mshahara baada ya kustaafu,na kutofautiana kwa sababu ya kustaafu kati ya nyaraka halisi na mfumo wa utumishi huku juhudi zikiendelea kufanyika ili kutatua mapungufu hayo ili wanachama waweze kupata mafao kwa mujibu wa sheria.
Bi.Chiume ameongeza kuwa baada ya mifuko ya PPF ,LAPF,GEPF,na PSPF kuunganishwa na kuundwa PSSSF tarehe 1,Agost,2019 serikali inafanya tathmini juu ya Mafao ya Uzazi na tathmini hiyo ikikamilika taarifa itatolewa kwa umma .
Kuhusu mfumo wa Malipo wa Government Electronic Payment Gatway[GePG] Bi.Chiume amesema umeleta faida kwa mwajiri kujifanyia tathmini ya michango inayotolewa na PSSSF ,Kujitengenezea Ankara za malipo ,kutengeneza control number,kuweka hesabu sawa,kuweza kupata risiti kwa wakati,kupunguza safari za kwenda kwenye ofisi za mfuko.
Na Faida kwa Mfuko ni kuongeza uwazi,ufanisi,kukusanya michango kwa wakati,mawasiliano rahisi na kutambua wanaowasilisha michango kwa wakati.
Pia ,Bi.Chiume amegusia juu ya suala la mfumo wa Majalada ya kielektroniki [Paperless Work Envinronment ]ambapo mfuko wa PSSSF Umeanza kutumia mfumo huo kwa kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali na kuongeza ufanisi na kupunguza matumizi ya karatasi.
Sanjari na hayo ,katika kueneza elimu kwa umma,PSSSF imeshiriki katika maonesho 43 ya kimataifa ya Dar Es Salaam na Jumla ya Wastaafu 381 na wanachama na wananchi wengine 1,040 walihudumiwa huku mfuko huo wa PSSSF Ukitarajia kushiriki kutoa huduma na Elimu kwa wananchi kwenye maonyesho ya Wakulima Nanenane Agosti 1 hadi 8 ,2019 yatakayofanyika katika eneo la Nyakabindi ,Bariadi ,Simiyu huku maonesho mengine ya PSSSF yakitarajia kufanyika katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya na Morogoro.
0 comments:
Post a Comment