Nimeulizwa kuhusu swali hili mara nyingi sana. Watu wengi sasa wanataka kusikia kutoka kwangu kuhusu viumbe hawa wa kipekee.
Kwa sababu siwezi kumjibu mtu mmoja mmoja leo nimeamua kutoa majibu ya ujumla kwa watu wote.
SAMAKI MTU NI NINI?
Samaki mtu ni jinni wa baharini ambae hujidhihirisha katika ulimwengu wa nyama kupitia ‘ masafa’ ya umbo la mchanganyiko wa samaki na mwanadamu.
Kuna sababu kubwa sana na ya msingi kwa nini jinni huyu hujidhihirisha katika umbo la samaki na mtu.
Labda tu kwa wale wasio fahamu, majini wanapo amua kujidhihirisha katika ulimwengu wa nyama na damu huwa wanafanya hivyo kwa kutumia ‘masafa’ ya wanyama mbalimbali kama vile nyoka, paka, nge nakadhalika. Ndio maana nyoka wengi wana tabia za kupotea potea kila wanapo onekana. Mnaweza kuwa mmekaa nyumbani akatokea nyoka mkaanza sekeseke la kumpiga, mara kaingia uvunguni mara ghafla haonekani, mkiona hivyo basi kuna uwezekano mkubwa sana nyoka huyo alikuwa jinni. Haya sasa tuendelee na samaki mtu.
SAMAKI MTU WANAPATIKANA WAPI ?
Samaki mtu wanapatikana baharini.
UMESEMA SAMAKI MTU WANAPATIKANA BAHARINI LAKINI MBONA KILA MARA HUWA TUNAENDA KUOGELEA BAHARINI NA HATUJAWAHI KUONA SAMAKI MTU HATA SIKU MOJA ?
Huwezi kuwaona samaki mtu ufukweni. Ndani ya bahari Samaki mtu hupatikana kwenye maeneo yenye vina virefu. Hata siku moja huwezi kumuona samaki mtu maeneo ya ufukweni. Majini wote wa baharini wenye nguvu za juu au wale walio katika daraja la juu, huwa wanapatikana kwenye sehemu zenye vina virefu.
Kamwe huwezi kuwaona ufukweni. Hata hivyo, majini walio katika koo nyinginezo za majini wanaweza kuonekana ufukweni kwa sababu maalumu sana lakini sio Samaki mtu.
Samaki mtu hawezi kuonekana ufukweni hata itokee nini!!! Na akitokea ufukweni labda uwe ni ufukwe ulio kwenye kisiwa kilichopo kati kati ya bahari kwenye kina kirefu na pili katika kisiwa hicho kusiwe na shughuli yoyote inayo muhusisha mwanadamu. Ipo sababu ya msingi sana ambayo ina mfanya samaki mtu asionekane ufukweni hasa hasa katika ufukwe ambao una tawaliwa na pilika pilika za mwanadamu.
UMESEMA SAMAKI MTU HAWEZI KUONEKANA WALA KUTOKEA KWENYE UFUKWE WENYE SHUGHULI NA PILIKA PILIKA ZA BINADAMU. SABABU NI NINI ?
Kuna sababu kuu mbili katika hili, lakini kabla sijaanza kuelezea sababu hizo ngoja nikukumbushe kitu kimoja muhimu sana. Baharini wanaishi majini waswafi tu. Baharini hakai jinni mchafu wa kisheitwani. Baharini hakikai kitu chochote kichafu. Ndio maana mtu akifariki baharini basi mwili wake unatupwa nchi kavu.
Uchafu ninao uzungumzia hapa ni uchafu wa kiroho yani kitu chenye nguvu hasi. Hata ndugu zangu wavuvi wakiwa kwenye shughuli zao baharini wanajua kwamba hawatakiwi kuingia kwenye shughuli wakiwa wachafu ( Mfano wakiwa na Janaba nakadhalika ). Sio hivyo tu, bali hata lugha wanayo takiwa kutumia wakiwa baharini inatakiwa kuwa lugha swafi na yenye staha. Hakuna lugha za matusi wala maneno ya hovyo baharini. Walio diriki kuzunguma maneno ya hovyo wakiwa baharini walipata habari yao.
Baharini kila kitu ni kisafi. Hata kwa wewe menye nuksi, balaa na mikosi ukienda kuoga maji ya baharini utaondosha nukushi zako zote, kwa sababu hakuna nguvu hasi inayo weza kukatiza baharini.
Sasa basi kama nilivyo sema hapo juu kwamba baharini hakikai kitu kichafu. Samaki Mtu ni jinni wa baharini. Ni jinni mswafi. Hakai na kitu kichafu. Sio tu kwamba ni jinni wa baharini bali pia ni jinni anae pendwa na majini wa baharini kuliko jinni mwingine yoyote yule.
Kila jinni wa baharini anampenda jinni huyu. Ni jinni mwenye kuwavutia sana majini wa baharini. Popote anapokuwa anatembea jinni huyu huwa anafuatwa na jinni kutoka katika kila koo ya majini wanao patikana baharini.
Kwa hiyo popote anapokuwa jinni huyu huwa ana ambatana na majini wa aina zote wa baharini. Ni mfano wa ndege wa porini aitwae Msese (Yule mwenye mkia mrefu) ambae kila mahali anapokwenda hufuatwa na kundi la ndege lakini , Samaki Mtu ni zaidi ya Msese kwa sababu Msese hufuatwa na ndege lakini sio ndege wote.
Ni kama ndege mmoja wa porini anae patikana kwa wingi huko kusini mwa Tanzania. Ndege huyo anapo taka kujenga kiota chake, kila ndege unae mjua wewe hupeleka jani kwa ajili ya kujenga kiota cha ndege huyu mwenye maajabu. Ninaposema ndege wote namaanisha ndege wote, kuanzia ndege warukao mchana hadi wale warukao usiku.
Kwa wanyama wanao patikana nchi kavu, jinni huyu naweza kumfananisha kidogo na mnyama aitwae Ngekewa( Mnyama wa porini anaependwa na kuhusudiwa na wanyama wote )
SABABU KWA NINI SAMAKI MTU HAWEZI KUONEKANA UFUKWENI, HASAHASA KWENYE UFUKWE WENYE SHUGHULI NYINGI ZA MWANADAMU.
Katika ulimwengu wa kiroho, samaki mtu ni kiumbe mwenye uhusiano mkubwa sana na mwanadamu. Na ndio maana anapo jidhihirisha katika ulimwengu wa nyama hujidhihirisha katika umbile la mwanadamu na samaki. Kuna maana na sababu kubwa sana katika hili.
Katika uliwmengu wa kiroho lipo jambo moja la rohoni ambalo samaki mtu anafanana sana na binadamu. Nalo ni asili ya NAFSI zao. Asili ya nafsi ya mwanadamu ni UMEME-SUMAKU. Yani ni umeme wenye sumaku yenye uwezo wa kuvuta na kukusanya vitu mbalimbali. Ndio maana kijana mwenye tabia nzuri anapo anzisha urafiki na kundi la vijana wenye tabia mbaya baada ya muda Fulani na yeye ataanza kuwa na tabia mbaya kwa sababu nafsi yake itakamatana na nafsi za vijana hao wenye tabia zisizo faa ( Ndio maana mzazi unashauriwa kuchunga sana aina ya marafiki wanao ongozana na mtoto wako )
Hii ni kwa sababu nafsi za mwanadamu zina tabia ya KUKAMATANA NA KUSHIKAMANA. Na ndio sababu wapenzi wakiachana nafsi zao huwa zinapata tabu sana. Humuwia vigumu sana mtu kuishi bila mpenzi wake ambae wamezoeana na nafsi zao zimekatana.
Vivyo hivyo na kwa samaki mtu. Asili ya nafsi ya samaki mtu ni UMEME-SUMAKU. Nafsi hii inaweza kukamatana na nafsi ya mwanadamu.
Samaki mtu anapokuwa katika mazingira yenye watu, nafsi yake huvuta na kukamata MAWAZO na FIKRA za watu wote waliopo katika eneo hilo kwa wakati huo jambo ambalo humletea shida sana kwa sababu nafasi ya mwanadamu inatawaliwa na mambo ambayo hayatakiwi kukaa kwenye nafsi ya samaki mtu.
Nafsi ya mwanadamu inatawaliwa na mambo makuu yafuatayo:
1. MAWAZO MACHAFU : Asilimia kubwa ya mambo anayo yawaza mwanadamu ni MAWAZO MAOVU. Uzinzi, uasherati, husda, kijicho, usengenyaji, wivu nakadhalika. Haya ni mawazo machafu ambayo hayatakiwi kukaa ndani ya nafsi ya Samaki mtu wala nafsi ya kiumbe yoyote wa kiroho aishie baharini.
Na sababu nimesha ielezea hapo juu. Baharini hakikai kitu kichafu. Nafsi ya samaki mtu haikai na kitu kichafu. Kwa kuwa Samaki Mtu hapendi na hawezi kukaa na vitu vichafu. Vitu vinavyo weza kunajisi nafsi yake, kiumbe huyu hukaa mbali kabisa na mahali wanapo kaa wanadamu kwa sababu ya kulinda usafi wa nafsi yake.
Samaki mtu hujisikia vibaya sana kuona viumbe wanao fanana na wao ( Yani sisi binadamu ) na ambao wapo katika daraja la juu sana la kiroho miongoni mwa viumbe wanaoishi duniani ( Binadamu ndio kiumbe wa Mwenyezi Mungu alie katika daraja la juu kabisa la kiroho miongoni mwa viumbe wote walioumbwa nae ) akiwa amebeba mambo machafu yasiyo endana na hadhi yake ya kiroho.
Mfano wake ni sawa tu na wewe mwanaume rijali ambavyo huwezi kukaa sehemu moja na wanaume mashoga na kusikiliza mambo wanayo yaongea. Watazungumza mambo yatakayo ichefua sana nafsi yako. Utahuzunika sana kuona wanaume kamili kama wewe wakiwa wanawaza mambo yaliyo kinyume. Na kitu kikubwa utakacho weza kukifanya ni kuondoka katika eneo hilo. Hutotaka kabisa kukaa karibu na watu hao. Ndivyo ilivyo kwa samaki mtu.
2. MAWAZO YA MAHANGAIKO NA HUZUNI YA MWANADAMU Nafsi ya mwanadamu pia imetawaliwa na huzuni nyingi. Magonjwa yasiyo pona, maradhi ya kichawi, ugumu wa kupata rizki, matatizo katika ndoa , hofu, mashaka nakadhalika ni mambo yaliyo tawala nafsi za wanadamu. Samaki mtu anapokaa katika eneo lenye watu wengi huweza kuvuta na kukamata mawazo haya ya huzuni yaliyo tawala nafsi za wanadamu.
Mawazo haya kwanza humtia huzuni sana kiumbe huyu kuona viumbe wanao fanana na yeye wakiwa katika mahangaiko na mateso makubwa. Huzuni, hofu, mashaka na kadhalika ni mambo ambayo hayatakiwi kukaa kwenye nafsi ya Samaki Mtu kwa sababu kiumbe huyu ameumbwa kuwa na furaha wakati wote. Huzuni hizo za wanadamu huchefua nafsi yake na kuisononesha. Kuepukana na kadhia hiyo, kiumbe huyu hapendi kabisa kukaa karibu na wanadamu.
Mfano wa huzuni na sononeko analo lipata hapa ni hapa ni ule ambao unaupata wewe mwanadamu ( mwenye moyo swafi ) ukimuona binadamu mwenzako akiwa kwenye matatizo makubwa. Mfano imetokea ajali watu wamepondwa pondwa na gari wamekufa vibaya. Kuna watu yakitokea matukio kama haya huwa hawataki hata kuangalia na kama ni kwenye TV huwa wanazima kabisa.
Mfano mwingine ni kuona maiti za binaadamu wenzako. Watu wengi wana hofu ya kutazama miili ya marehemu na ni wachache wanaweza kusogea na kukaa sehemu ambazo kuna miili ya watu walio kufa.
Kuona maiti ya mtu unaempenda sana. Watu wengi hushikwa na huzuni sana pindi wanapo ona maiti za watu wao wa karibu. Huhuzunika sana hutamani wasione kabisa. Ndivyo ilivyo kwa samaki mtu. Ndio maana hawapendi kukaa karibu na mahali walipo binadamu.
UMESEMA SAMAKI MTU WANAPATIKANA KWENYE VINA VIREFU BAHARINI LAKINI MBONA HUWA TUNAPITA KWENYE MAENEO HAYO LAKINI HATUWAONI?
Huwezi kumuona Samaki Mtu kwa sababu yupo katika ‘masafa’ tofauti na masafa uliyopo wewe. Hwezi kumuona kwa macho ya nyama na damu.
Viumbe tuliopo duniani tunaishi katika masafa tofauti tofauti. Ndio maana viumbe wengine mfano majini hawaonekani kwa sababu wapo kwenye masafa tofauti na binadamu ingawa tunaishi nao katika dunia hii hii.
Mfano wake ni sawa na redio yako . Ukiwa na redio yako ukiweka mfano masafa namba moja unapata matangazo ya redio Fulani, ukiweka masafa namba mbili unapata matangazo ya redio nyingine nakadhalika nakadhalika.
Ndivyo ilivyo kwa binadamu na majini. Tunaishi nao majumbani mitaani, tunapishana nao barabarani, njia panda, vyooni, makaburini nakadhalika lakini huwezi kuwaona kwa macho ya damu kwa sababu wao wapo kwenye masafa ya juu kuliko masafa yako mwanadamu.
Vivyo hivyo kwa samaki mtu. Huwezi kumuona kwa macho ya damu na nyama kwa sababu yeye ni jinni na yupo Kwenye masafa tofauti na masafa ulyopo wewe.
JE NIKITAKA KUMUONA SAMAKI MTU NINATAKIWA KUFANYA NINI ?
Ukitaka kumuona samaki mtu kwanza unatakiwa kuwa katika masafa yake . Yani kuwa na uwezo wa kuona vitu visivyo weza kuonekana kwa macho ya nyama na damu. Unaweza kupata uwezo huo kwa kufanya mambo yafuatayo : Kwanza hakikisha una moyo mswafi. Yani ndani ya nafsi yako usiwe na wazo lolote hasi. Uzinzi, uasherati,. Husda, kisasi, kinyongo nakadhalika. Pili usiwe na uchungu wala huzuni ya kiwango chochote ndani ya nafsi yako. Uwe na moyo wenye furaha wakati wote. Tatu usiwe na tamaa ya kupata chochote . Yani lengo lako liwe tu unataka kumuona tu jinsi alivyo na sio unataka kumuona kwa ajli ya kupata faida yoyote kutoka kwake.
Baada ya hapo uende kwenye kisiwa kilichopo baharini . Kisiwa kiwe kwenye kina kirefu na kusiwe na shughuli zozote za binadamu katika eneo hilo. Baada ya kufika kwenye kisiwa hicho, utafunga na kufanya dua ya kuomba kumuona kiumbe huyu. Ikiwa ni bahati yako kiumbe huyu atakutokea na utamuona. Na asipo kutokea laivu basi anaweza kukutokea katika ndoto.
Kama unaona itakuwa vigumu kwenda kwenye kisiwani unaweza kufanya ombi maalumu la kumuona Samaki huyo katika ndoto. Utatakiwa kutimiza vigezo vyote nilivyo vitaja hapo juu yani uwe na moyo mswafi, usiwe na huzuni ( uwe na furaha wakati wote ) na usisukumwe na tamaa ya kupata kitu chochote kutoka kwa samaki huyo.
Kila siku utakuwa unaenda ufukweni. Utakuwa unaingia kuogelea kama waingiavyo watu wengine na ukiwa ndani ya maji uwe una fanya maombi yako yani uwe unaomba kuonyeshwa Samaki Mtu kupitia ndoto.
Ufanye hivyo bila kuchoka wala bila kuwa na haraka ya kupokea majibu yako. Baada ya muda Samaki huyu atakutokea katika ndoto. Utamuona Katika ndoto. Kama ni bahati yako basi atakutokea katika ndoto baada ya muda mfupi lakin, Inaweza kukuchukua siku arobaini, inaweza kuchukua miezi mitatu, miezi sita, mwaka mzima, miaka mitatu hata Zaidi ya hapo. Utakacho takwa kufanya ni kuwa mvumilivu. Na kadri utakavyo kuwa mvumilivu ndivyo utakavyo kuwa katika nafasi nzuri ya kumuona samaki huyo.
· Je Samaki Mtu wanaongea ?
· Kama wanaongea huwa wanaongea lugha gani ?
· Ni kweli samaki mtu huwa wanasuka nywele zao ?
· Ni kweli samaki mtu huwa wana wabembeleza na kuwanyonyesha watoto wao ?
· Je kuna uhusiano wowote ule wa vinasaba vya kiroho kati ya Samaki Mtu na Mwanadamu ?
· Kuna dawa moja ya asili inajulikana kama AMBARI NYEUPE YA BAHARINI. Dawa hii inatumika kufungua vifungo vya aina zote na kuwafukuza majini wabaya mwilini,kwenye biashara na kwenye miji . Lakini pia dawa hii inatumika katika tiba ya kurefusha na kunenepesha maumbile ya kiume. Kuna watu wanasema dwa hii inatokana na nyangumi na wengine wanasema dawa hii inatokana na Samaki Mtu. Je Ukweli ni upi ?
Yote haya nimeyaelezea kwa undani sana kwenye kitabu changu kiitwacho " MESENJA WA BAHARINI " ambacho kitakuwa mitaani kuanzia tarehe 01 SEPTEMBA 2019.
Kitabu kitapatikana nchi nzima kwenye maduka ya kuuza vitabu pamoja na kwenye vibanda vya wauza magazeti. Nchi jirani kitabu hiki kitapatikana pia Mombasa, Nairobi na Lamu nchini Kenya.
Mbali na kuelezea kwa kina kuhusu Samaki Mtu,ndani ya kitabu hiki utapata kujua kuhusu vitimbi mbalimbali vinavyo watokea binadamu wakiwa baharini pamoja na mambo yote muhimu yanayo husiana na ufalme wa baharini.
IMESIMULIWA NADOKTA. MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KUPITIA SIMU NAMBA 0744 - 000 473.
0 comments:
Post a Comment