Thursday 18 July 2019

BENKI YA STANDARD CHARTERED YALETA HUDUMA MPYA YA SC KEYBOARD BANKING

...
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba (kulia) akitoa utambulisho wa meza kuu kutoka kulia kwake ni Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki hiyo, Bw. Ajmair Riaz pamoja na Mkuu wa Teknolojia wa benki hiyo Bw. Christopher Vuhahula wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard Banking uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt-Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya SC Keyboard ya Kibenki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba (kulia).
 Mkuu wa Teknolojia wa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Christopher Vuhahula akielezea kuhusu huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz

 Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kupeleka habari njema kwa umma wa watanzania wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki uliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ajmair Riaz, Mkuu wa Teknolojia wa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Christopher Vuhahula (kushoto) pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba (kulia).
 Meneja Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Ndibalema Rwezaura akielezea jinsi huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki inavyofanyakazi kwa urahisi kupitia simu ya kiganjani wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa bidhaa hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Meneja Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ndibalema Rwezaura (kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wenzake Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Bi. Mariam Sezinga (katikati) pamoja na Meneja Masoko wa benki hiyo, Bw. Wilfred Nyakyi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt-Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee.
 Picha ya pamoja huku fataki zikiwaka kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya Kibenki kwa wateja wa Benki ya Standard Chartered kutoka kushoto ni Meneja Bidhaa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Ndibalema Rwezaura, Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee, Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi. Juanita Mramba, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki hiyo, Bw. Ajmair Riaz pamoja na Mkuu wa Teknolojia wa benki hiyo Bw. Christopher Vuhahula  katika hafla fupi iliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt-Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

 Picha ya pamoja kutoka kushoto ni Mkuu wa Teknolojia wa wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Christopher Vuhahula, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki hiyo, Bw. Ajmair Riaz, Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Bi. Juanita Mramba mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee wakiwa na Antu Mandoza wa Radio 7 mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Huduma za Kibenki za Kidigitali wa Benki ya Standard Chartered, Vanessa Mdee katika picha ya pamoja na Antu Mandoza wa Radio 7 mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya SC Keyboard ya kibenki iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Benki ya Standard Chartered imezindua kwa mara ya kwanza huduma mpya katika soko la fedha nchini. Uwapo wa bidhaa hiyo ni juhudi za benki kulihudumia soko la fedha kwa njia ya mtandao linalokuja juu kwa sasa.

Huduma hiyo inayojulikana SC Keyboard Banking inatoa nafasi ya matumizi ya mitandao ya simu katika mitandao ya kijamii kupata huduma mbalimbali za kifedha. Huduma hiyo ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya utoaji huduma kwa simu kupitia benki ya kidijiti.

Huduma hii ambayo imezinduliwa nchini Tanzania, ipo nchini Kenya, Uganda na Ghana.
Huduma hii kupitia mitandao ya kijamii ni ya kwanza kwa benki katika bara la Afrika na kwamba  zinatarajiwa kupelekwa nchini Botswana, Zambia, Zimbabwe na Nigeria kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Watumiaji wa Huduma hiyo watakuwa na uwezo kusafirisha fedha kwa muda huo huo na kufanya malipo mengine na kuangalia salio kwa kutumia mtandao wa kijamii au jukwaa. Upekee wa huduma hiyo ya kidijiti unatokana na ukweli kuwa mtumiaji anaweza kufanya kuwa chaguo la msingi katika simu yake na hivyo kuwa na kasi katika kupata huduma ya kibenki bila kujiingiza katika applikesheni za benki ya kidijiti (SC Mobile App) kupata huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Wateja wa Kawaida wa Benki hiyo, Bw. Ajmair Riaz, alisema kwamba kuwepo kwa Huduma hiyo ya SC Keyboard Banking ni hatua muhimu katika safari ya kidijiti ya benki hiyo. Alisema kwamba huduma hiyo imebuniwa kwa kuzingatia maslahi ya wateja ambapo wateja sasa wanaweza kulipa tozo mbalimbali, kuangalia akaunti zao na kusafirisha fedha kupitia mitandao ya kijamii iwe ni kwenye Whatsup, Instagram, Facebook, Messenger au njia ya kawaida ya ujumbe mfupi (SMS). 

“Tunataka shughuli hii iwe nyepesi na rafiki na kwamba tupo tayari kuendelea kutumia teknolojia ya kisasa ili kuwezesha shughuli za kibenki kuwa za kisasa zaidi na zinazozingatia mahitaji ya wateja.” alisema. Naye Mkuu wa Teknolojia katika benki hiyo Bw. Christopher Vuhahula, alisema wataendelea kuimarisha ubunifu katika teknolojia ya dijiti katika huduma za fedha.

Balozi wa bidhaa hiyo Vanessa Mdee amesema amefurahishwa mno kujihuisha na huduma hiyo na kuwataka mashabiki wake kutumia huduma hiyo kurahisisha maisha yake. “Kama wapenzi wangu mnavyojua, mimi ni mtumiaji mzuri wa simu lakini SC Keyboard Banking ina niruhusu kuendelea kuchati huku naendelea na shughuli zangu za kifedha, imefanya maisha kuwa rahisi zaidi”  alisema Vanessa.

Katika masuala ya dijiti Standard Chartered’ ina aplikesheni inayoitwa “SC Mobile Tanzania App” kwa kupitia Playstore au AppStore.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger