Friday, 4 January 2019

WAZIRI UMMY ATOA MABATI 100 KATA YA KIRARE JIJINI TANGA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI

...

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi mabati 100 Diwani wa Kata ya Kirare Jijini Tanga Mwagilo ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare wanaoshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudu Mayeji kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga wa Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni mara baada ya kukabidhi mabati hayo wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
 Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kwa umakini Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kukabidhi mabati 100
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto akikagua dawa kwenye zanhanati ya Mapojoni wakati alipokwenda kuwakabidhi mabati 100 
 ***
Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekabidhi mabati 100 katika Kata ya Kirare Jijini Tanga kwa ajili ya zahanati za Mapojoni na Ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Kirare.

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu umbali wa kilomita 15 jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao. 

Halfa ya makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye Kata hiyo ikiwa ni juhudi zinazoonyeshwa na Mbunge huyo
kwa ajili ya kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananachi anashirikiana nao kuweza kuzipatia ufumbuzi. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mabati hayo Waziri Ummy alisema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziweze kupata ufumbuzi.

Sambamba na Waziri huyo kuchangia mabati hayo wakati huo
huo Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imeguswa na changamoto hiyo na kuchangia mabati 50 na saruji 70 katika ujenzi wa bweni la wasichana la shule ya Sekondari Kirare na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi. 

Alisema kwani wao watahakikisha wanashirikiana na wananchi kwenye maeneo mbalimbali kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto za Afya ambazo zinaweza kuwa kikwazo kwenye kujiletea maendeleo. 

“Labda niwaambie tu kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Magufuli imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha changamoto mbalimbali zinbapatiwa ufumbuzi
hivyo endeleeni kushirikiana nayo kuweza kupata mafanikio ",alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri huyo alisisitiza umuhimu wa wananchi kuhakikisha wanakata bima za Afya ili ziweze kuwasaidia kunufaika na huduma za matibabu wanapokuwa wakiugua. 

“Niwasisitize kwamba kateni bima ya Afya mkiumwa muweza kupata huduma za matibabu kwani wengine fedha zenu ni za msimu hivyo mkiwa na bima mnaweza kupata matibabu bure”,alisema. 

Waziri huyo alisema gharama za matibabu zimekuwa kubwa hivyo iwapo wakijiunga na bima hususani iliyoboreshwa ukitoa elfu thelathini kwa kaya ya watu sita unaweza kupata huduma za matibabu kwenye maeneo mbalimbali. 

“Bima kubwa ya kitaifa ya NHIF wana bima ya mtoto wameona badala ya kusema mtoto aishie elfu thelathini tu kwa hiyo ukimliptia mtoto 50400 atapata huduma mzuri”,alisema. 


Alisema sababu ya kusaidia juhudi hizo za wananchi ni kutokana na kuguswa namna walivyojitahidi kuhakikisha wanajenga jengo hilo wakishirikiana na viongozi wenu namna hivyo kuamua kuwaunga mkono. 

Aidha alisema anaamini mabati hayo yatakuwa chachu katika
 kutatua changamoto iliyopo kwenye jengo hilo ili kuweza kuzimaliza na kutoa fursa kwa wananchi kuweza kupata huduma bila kuwepo vikwazo. 

“Lakini hapa nimeambiwa mnachangamoto ya vifaa hivyo
 nitashirikiana nanyi kuweza kuzipatia ufumbuzi vifaa vyote
vinavyoihitaji kwenye zanahati hii”,alisema 

Awali akizungumza,Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Isango Isubiri alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fedha za ukarabati za vituo vya afya kwenye Jiji ambavyo ni Makorora,Ngamiani,Mikanjuni na Duga ambao kwa sasa unaendelea. 

Alisema kwenye zahanati ya Mapojoni Jijini Tanga kulikuwa na uhaba wa chumba cha maabara na daktari hivyo kilichofanywa na Waziri huyo ni kutambua umuhimu kuunga mkono nguvu
za wananchi katika ujenzi wa jengo hilo lenye uhitaji mkubwa ambalo baada ya kulijenga walikosa mabato na saruji ili kuweza kulikamilisha.

Mganga huyo wa Jiji alisema ujenzi wa Jengo hilo ulianza mwaka 2016 ambapo litakapokamilika litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi ambao wanakwenda kupata huduma za matibabu kwenye zahanati hiyo. 

Aidha alisema pia suala lingine ni ujenzi wa hospitali ya
wilaya ya Tanga ambapo zilitolewa Bilioni 3.6 katika kipindi cha mwaka 2018 jambo ambalo limesaidia kuweza kuondosha changamoto ya afya. 

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger