Tuesday 22 January 2019

WAZIRI LUGOLA ATAJWA KUTETEA WATUHUMIWA

...
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepongezwa kwa hatua yake ya kuwatetea baadhi ya watuhumiwa ambao wamekuwa hawatendewi haki pindi wanapokuwa mikononi mwa jeshi la polisi.

Wakitangaza uamuzi Jijinji Dar es salaam Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRDC) pia walitangaza kuanzishwa kwa operesheni maalum iliyopewa jina la Tetea haki za Watuhumiwa lengo ni kuwatetea watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumo amesema, "tunampongeza Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kujitokeza kuwatetea baadhi ya watuhumiwa nchini".

"Kwa mujibu wa sheria jeshi la polisi lina wajibu wa kumpa mtuhumiwa haki yake ya kupata msaada wa kisheria kitu ambacho kwa Loliondo imekuwa shida na hii ni kwa maeneo yote ya vijijini siyo Loliondo pekee", ameongeza Onesmo Olengurumo.

Mara kwa mara Kangi Lugola amekuwa akiwachukulia hatua baadhi ya Makamanda wa Polisi ambao wamekuwa hawatoi haki kwa wartuhumiwa wa matukio mbalimbali ya kiuhalifu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger