Watu wawili wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongwa na gari la polisi wilayani Monduli mkoani Arusha.
Tukio hilo limetokea jana jioni Januari 3, 2019 eneo la Meserani Duka Bovu wilayani Monduli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
"Ni kweli kuna hiyo ajali lakini mkuu wa upelelezi mkoa amekwenda eneo la tukio ndio atatupa taarifa sahihi ya kilichotokea,” amesema.
Kamanda Ng'azi amesema taarifa sahihi za tukio hilo ikiwepo majina ya marehemu zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Pikipiki hiyo ilikuwa ikitoka kuweka mafuta katika kituo cha mafuta kilichopo pembezoni mwa barabarani ya Arusha- Dodoma na kukutana na gari hilo lililokuwa likipita barabara kuu.
0 comments:
Post a Comment