Brian Colaneri na Andrew Crysel (kushoto kwenda kulia) pamoja na mvulana wa miaka 16 wanashitakiwa kwa kupanga shambulizi la mabomu dhidi ya Waislamu.
Watu wanne wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kupanga shambulio dhidi ya jumuiya ndogo ya waislamu katika jimbo la New York.
Watu hao wanatuhumiwa kukutwa na mabomu ya kungeneza nyumbani na silaha za moto, na kupanga kushambulia jumuiya ya Islamberg iliyoanzishwa na kiongozi wa dini kutoka Pakistani kwenye miaka ya 80.
Njama hizo zilibainika baada ya polisi kupashwa habari na mwanafunzi.
Watuhumiwa watatu Andrew Crysel, 18, Vincent Vetromile, 19 na Brian Colaneri, 20, wanatarajiwa kupandishwa mahakamani leo Jumatano.
Kwa mujibu wa polisi, watatu kati ya watuhumiwa hao walikuwa pamoja katika mafunzo ya uskauti.
Wapelelezi wanasema watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiishi katika jiji la Greece, kaskazini-magharibi mwa jimbo la New York walikuwa wametengeneza mabomu matatu na walikuwa na silaha 23 walizozificha katika sehemu tofauti.
Chanzo:Bbc
0 comments:
Post a Comment