Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Rashid Mfaume ameeleza juhudi zinazofanywa na serikali kuzuia vifo vinavyosababishwa na uzazi kwa uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya afya.
Mfaume ameeleza mwenendo wa vifo vya watoto wachanga kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 mpka 2018, na kusema mwaka 2015 vifo vya watoto wachanga vilikuwa 1340 na mwaka 2018 kushuka hadi 815 kutokana na juhudi za uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya afya licha ya changamoto zinazojitokeza ikiwemo ukosefu wa elimu kuhusu afya ya mama na mtoto.
Amesema vifo hivyo vinasababishwa na mzazi kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua,kifafa cha uzazi na kupasuka kwa kizazi jambo ambalo baadhi ya wanajamii wamekuwa wakidhani kurogwa na kuamua kutafuta matibabu kwa waganga wa jadi badala ya kwenda kwenye vituo vya afya kupata matibabu ama ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.
“Kuna vifo vingi vinavyosababishwa na uzazi vinatokana na baadhi ya vituo vya afya kukosa vitendea kazi , na wengine kuwa na tatizo la upungufu wa damu,hivyo wadau wa afya tukishirikiana kwa pamoja kuhamasisha jamii kujua umuhimu wa mama mjamzito kujifungua katika vituo vya afya itasaidia kupunguza vifo hivyo,” Alisema Mfaume
Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment